Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Khamis Hamza Khamis amewataka wawekezaji wanaofanya shughuli za uzalishaji kwenye vyanzo vya maji kuhakikisha wanatii sheria kwa kutunza vyanzo vya maji.
Khamis ametoa agizo hilo alipotembelea kampuni ya Tangreen Agriculture Limited kinachojishughulisha na uvuvi wa samaki kwa njia ya vizimba kilichopo Kijiji cha Kigangama Kata ya Kitongosima Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Mwanza.
Katika hatua nyingine naibu waziri Khamis amewataka wawelezaji wote nchini wanaojenga viwanda ambavyo vinatumia moto kuyeyusha malighafi watumie teknolojia mpya zinazothibiti kelele na moshi ili kutowapa athari wananchi.
Agizo hilo pia amelitoa jijini Mwanza na alipotembelea ujenzi wa kiwanda cha Ziwa Steel And Wire Product kitakachotengeneza nondo na mabati kilichopo Kata ya Nyanguge Tarafa ya Kahangala Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza.
0 Comments