Header Ads Widget

MWANAHARAKATI ATOA USHAURI KWA SERIKALI KAMPUNI ZINAZOJIHUSISHA NA MAGENDO ZIFUTWE.

 


NA THABIT MADAI, ZANZIBAR - MATUKIO DAIMA APP.

MWANAHARAKATI wa Haki za Binadamu na Utawala Bora, Ali Makame Issa amesema kampuni za vileo zinazojihusisha na biashara za magendo zinapaswa kufutwa ili kulinda upotevu wa mapato ya Serikali visiwani Zanzibar.

Amesema, fedha nyingi za Serikali ambazo zingetumika kuleta Maendeleo kwa Wananchi zinapotea kutokana na baadhi ya kampuni kujihusisha na Magendo

Wito huo ameutoa leo Wakati akizingumza na Waandishi wa Habari  umetolewa na mwanaharakati huyo katika ukumbi wa jumuiya ya watu wasiona Zanzibar, kuhusu sakata la kampuni ya MGW 2014 Enterprises kutuhumiwa kuingiza vileo vya magendo Febuari 12 mwaka huu na kuhifadhiwa katika ghala la kampuni hiyo, Amani Mkoa wa Mjini Magharib Unguja.

"Serikali inapaswa kuwa Makini na kuzifuta  Kampuni ambazo zinajihusisha na Magendo na kuingiza Vileo kinyume na Utarabu na kukosesha Serikali pato lake," Amesema.

Amesema kwa mujibu wa sheria kampuni zilizopewa vibali vya kuingiza pombe Zanzibar baada ya kushinda sifa na masharti ya dhabuni ni kampuni tatu ikiwemo Scoch, one stop na ZMMI ambao ndio waingizaji pekee.

Hata hivyo amesema kwamba pamoja na kampuni hizo kuruhusiwa kisheria, lakini kuna taasisi moja ya ulinzi na usalama nayo imekuwa ikiingiza vileo.

Aidha mwanaharakati huyo amesema, kwamba lengo la kutungwa sheria ya vilio ya mwaka 2020 ililenga kuziba mianya ya ukwepaji wa kodi kupitia biashara ya vileo pamoja na uingizaji holela wa pombe Zanzibar.

Hata hivyo msimamizi wa kampuni ya MGW2012 Enterprise Ali Seif, amekanusha kampuni yake kuhusishwa na biashara ya magendo na kudai wamekuwa waksiambaza vileo baada ya kununua kutoka katika kampuni tatu zilizopewa vibali Zanzibar.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI