Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
MSEMAJI Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa amewataka waandishi wa habari mtandaoni kuzingatia uweledi na wasikubali kutumika na watu ama makundi yenye nia mbaya nao.
Msigwa aliongea hayoJijini Dodoma, wakati akizindua Taasisi ya Waandishi wa Habari Mtandaoni (TOMA) ambapo ameeleza kukubali kutumika kutapelekea kupoteza dhana ya uwepo na ukuaji wa sekta ya habari.
Aidha amesema katika nchi yetu tatizo lililopo ni Media house nyingi na weledi kwani kumeibuka watu ambao wanazusha tu habari bila kuzingatia maudhui fulani yatakuwa na matokeo gani kwenye jamii.
" Tujitahidi kujitofautisha na hao ili tulinde taaluma yetu ukweli ni kwamba Serikali inaona na kutatambua juhudi za vyombo vya habari na ndio maana imetoa uhuru wa kutosha kila mmoja kuanzisha na kumiliki chombo chake cha habari ," Amesema.
Na kuongeza"Licha ya kupewa Uhuru kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya Chombo vya habari kutokujua namna gani ya kuchuja kipi kiende hewani na kipi kisiende kulingana na maudhui yake,"amesema Msigwa
Kutokana na hayo amewataka wamiliki wa vyombo vya habari pia kuhakikisha wanazingatia weledi katika utendaji kazi wao hasa katika kipindi hiki cha Mapinduzi ya teknolojia ," Amesema Msigwa
Msigwa amesema kwa kutokana na kukuwa kwa matumizi ya TEHAMA imerahisisha habari kufika kwa jamii kwa haraka sana hivyo vyombo vya mitandaoni imekuwa tegemewe kama chanzo kikuu cha habari.
Hata hivyo Msemaji huyo wa Serikali amesema Tasnia ya Habari ipo mikononi mwa vyombo vya habari vya Mtandaoni, kwa sasa vyombo vya habari Mtandaoni vimekuwa nguzo kubwa kwa sekta ya habari nchini .
"Nimefarijika Sana kuona Chama hichi Cha TOMA kimeanzishwa kwani ninaimani kitakwenda kuhakikisha waandishi wa habari mtandaoni wanakuwa na uelewa mkubwa juu ya machapisho wanaotuma mtandaoni,"amesema Msigwa
0 Comments