Header Ads Widget

MBUNGE KIHENZILE AFANYA KUFURU JIMBONI AGAWA MIFUGO YENYE THAMANI YA SH.BILIONI 1.5 KWA WAPIGA KURA WAKE JIMBONI ..


MBUNGE wa Mufindi Kusini David Kihenzile ameendelea kufanya kufuru ya kimaendeleo Jimboni humo baada ya Kugawa mifugo  yenye thamani ya Sh bilioni 1.5  kwa wapi kura wake  ili kujikwamua Kiuchumi kupitia ufugaji huo .

Maeneo ambayo wananchi wameanza kupewa mifugo hiyo ni pamoja na Kata ya Nyololo na Maduma  ikiwa ni utekekezaji wa agenda ya 'One family one catle'.

Mbunge Kihenzile ametoa Mifugo hiyo Kwa ubia mkubwa wa  Shirika la World Vision ambalo limetoa  Ng’ombe 600, Nguruwe 600 na Kuku 4,000


Mbunge  Kihenzile amesema ugawaji wa wanyama hai kwa wananchi lengo ni kupambana na utapiamlo na kuimarisha lishe kwa wananchi na kukuza kipato Chao.

"Mifugo hii pia itasaidia kuongeza kipato kwa wananchi, kuhamasisha ulimaji wa nyasi za malisho hivyo kuzuia kilimo kwenye vyanzo vya maji, Samadi itatumika Shambani hususani kwenye Parachichi, Mahindi na mazao mengine."Amesema na kuongeza

"Pia ni maandalizi ya uzalishaji nishati ya Biogas, kutoa uhakika wa malighafi viwandani ikiwemo maziwa, ngozi, nyama pamoja na kwato."


Aidha, Kihenzile amewataka wananchi wa Mufindi Kusini kuunganisha nguvu katika kuboresha afya na uchumi.

Kihenzile pia amelishukuru Shirika la World Vision kwa kutoa wanyama wenye thamani ya Tshs 1.5bilion na pia kuwashukuru wadau wengine ambao wako kwenye Mkakati wa utekelezaji wa kuunga Mkono jitihada hizo ikiwa ni pamoja na Shirika la Land O’Lakes, Benki ya Kilimo, Water For Africa, Halmashauri ya Mufindi, aidha ameomba wadau wengine kuunga mkono Agenda hiyo ili kuweza kuwafikia wananchi mbalimbali kwenye Kata zote 16

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI