Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaApp NJOMBE
Duru zimearifu kuwa mateso ya miaka Saba ya vyama vya siasa nchini Tanzania kuzuiwa na kushindwa kukutana na wananchi kupitia mikutano ya hadhara pomoja na kukosa Uhuru wa kujieleza kwa mujibu wa ibara ya 18 ya katiba ya Tanzania yameanza kuisha baada ya Rais kukubali kuingia kwenye maridhiano na vyama hivyo.
Baadhi ya wananchi mkoani Njombe akiwemo Richard Mhema,Chezalina Mwelela na Vaileth Mhagule wametoa kauli hiyo baada ya mwenyekiti wa Chadema taifa kufanya mkutano wa hadhara katika eneo la kituo cha mabasi cha zamani mjini Njombe na kuwaeleza hali ya siasa hivi sasa na mustakabali wa vyama vya siasa.
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa chadema Taifa Freeman Mbowe ameonesha kushangazwa na kitendo Cha jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi katika mikutano yote ya chadema bila kuwabugudhi na kwamba Ni mabadiliko makubwa katika kipindi Cha miaka Saba ambayo ilikuwa Ni ya mateso makubwa kwao.
Pia Mbowe amesema wanaendelea na maridhiano na Rais juu ya kupata katiba mpya itakayopunguza mamlaka makubwa ya Rais pamoja na kudai tume Huru ya Uchaguzi.
Awali mwenyekiti wa chadema mkoa wa Njombe Rose Mayemba ametumia fursa hiyo kuomba maridhiano yasaidie kuwatoa gerezani wafungwa wa kisiasa waliokamatwa mwaka 2020 katika mkoa wa Njombe kwa tuhuma za mauaji.
Mwenyekiti wa chadema Jimbo la Njombe mjini Regnard Danda amesema wananchi wameendelea kupata mateso ya michango mingi kwa muda mrefu pamoja na adha inayotokana na Kituo Cha zamani Cha mabasi Cha Njombe mjini kuzuiwa.
Freeman Mbowe mwenyekiti wa Chadema Taifa februari 28,2023 ataendelea na mikutano ya hadhara kwa kuzungumza na wakazi wa mkoa wa Iringa.
0 Comments