NA HADIJA OMARY LINDI.....
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa leo ameshudia hafla ya Utiaji Saini mikataba wa ujenzi wa maji kwa vijiji 55 vya Wilaya za Nachingwea na Ruangwa Mkoani Lindi utakaoghalmu kiasi cha shilingi Bilioni 119.15 Baina ya wakala wa maji na usambazaji maji vijijini Ruwasa na wakandarasi wawili M/STC CONSTRUCTION COMPANY LIMITED na M/S. EMIRATES BUILDERS CONSTRUCTION. LIMITED
Akizungumza mara baada ya kushuhudia hafla hiyo iliyofanyika katika chuo cha ufundi stadi VETA Wilayani Ruangwa Waziri Mkuu Majaliwa alisema dhamira ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan ni kuendelea kumtua mama ndoo kichwani kwa kuhakikisha wananchi wote wa Mkoa wa Lindi na Taifa kwa ujumla wapata huduma ya maji safi na salama.
Mh Majaliwa amesema ndani ya Mkoa wa Lindi Miaka Miwili ya Mama Samia Suluhu Hassan kwenye Sekta hiyo ya maji zaidi ya Bilion 60.4 zimetumika kwa ajili ya usambazaji wa maji vijiji na mijini ili wananchi wapate huduma ya maji na wanawake kutotembea umbali mrefu Kutafuta maji kwa kuwa Serikali yao ipo kwa ajili ya kuwahudumia .
" Malengo ya Serikali yetu ya awamu ya sita ni kumtua mama ndoo kichwani kwa kumpatia maji safi na salama katika maeneo yote ya Taifa letu hivyo niwaombe wananchi na Watanzania kwa ujumla kulinda na kusimamia vyanzo vya maji kwa kuto fanya wizi wowote wa Vifaa vinavyowekwa hivyo tuwe mabarozi wazuri wa kulinda vyanzo vya maji katika maeneo yetu "
Hata hivyo Mh Majaliwa amewataka wakandarasi waliopewa tenda hii ya Ujenzi mradi wa maji ndani ya wilaya hizi mbili kuhakikisha wanasimamia kwa weredi Mradi huu ambao Serikali umeweza kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kuwapatia huduma bora wananchi .
Mh Majaliwa alisema ni jukumu la Ruwasa katika Mkoa huo wa Lindi kuwasimamia wakandarasi hao ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi ili wananchi wapate maji kwa haraka kwa kuwa Serikali imeshawapa fedha hizo kwa ajili ya Ujenzi .
Awali,Mkurugenzi Mkuu wa Ruwasa nchini mhandisi Clement Kivegalo akitoa taarifa ya mradi huo mbele ya waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema utakuwa na uwezo wa kuhudumia watu zaidi ya laki moja na thelathini wa vijiji hivyo na kuongeza wastani wa upatikanaji wa Maji kutoka asilimia 63 ya sasa hadi kufikia asilimia 85 na mradi huo mpya uliosainiwa unagharimu kiasi cha zaidi ya Bilion 120 huku ukitekelezwa kwa kipindi cha miezi 14.
" Mradi huu mpya ambao mikataba yake ya ujenzi itasainiwa muda mfupi ujao, chanzo chake ni Mito Nyangao na Chiue iliyopo Wilaya ya Lindi. Chanzo hiki kitakuwa na uwezo wa kuzalisha maji wastani wa lita 15,000,000 kwa siku, wakati mahitaji ya maji kwa vijiji vyote vilivyopangwa kuhudumiwa na mradi huu kwa miaka 20 ijayo ni wastani wa lita 6,912,000 kwa siku. Hivyo, chanzo cha mradi huu ni toshelevu kwa zaidi ya asilimia 100 kwa kipindi cha miaka 20 ijayo."
Alisema katika kuhakikisha kuwa mradi unatekelezwa kwa ufanisi ndani ya muda mfupi kadri inavyowezekana, mradi umegawanywa katika sehemu (Lots) mbili, ambapo kila sehemu itakuwa na mkandarasi wake ambapo Sehemu ya kwanza itahusisha ujenzi wa dakio la maji, ujenzi wa bomba kuu la maji mtiririko (gravity main) na maji ya msukumo (pumping main) jumla ya km 85 yenye ukubwa wa kipenyo cha mm 500 ambapo Sehemu hiyo itatekelezwa na Kampuni ya STC Construction Company Limited ya Dar Es Salaam kwa gharama ya Sh. 12,417,026,276.92 bila Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa muda wa miezi kumi nan ne (14).h
Aliongeza kuwa Sehemu ya pili ya mradi huo inayohusisha kazi zote zilizobaki, itatekelezwa na Mkandarasi Emirate Builders Co. Limited ya Dar Es Salaam kwa Sh. 107,138,897,161.00 bila Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa muda wa miezi ishirini na sita (26). Kampuni zote mbili ni za kitanzania.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack amesema kwa upande wa sekta ya Maji, Serikali ya awamu ya Sita imetoa fedha kiasi cha Tshs Billioni 26,267,162,121.23 kwa ajili ya uboreshaji wa huduma ya maji katika Makao makuu ya miji ya Wilaya na maeneo ya vijiji katika Manispaa ya Lindi na miji ya Ruangwa, Liwale na Kilwa imepokea kiaisi cha shillingi Tshs Billioni 10,276,622,307.00 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 4 ya maji.
Mh Telack amesema Fedha hizo pia zinahusisha kuongeza mtandao wa maji katika miji ya Mitwero, Mkwaya, Kitunda, Kiduni, Ngongo, Mayani na Mchinga katika Manispaa ya Lindi na Mradi mwingine unaokwenda sanjari na hiyo ni pamoja na uboreshaji mradi wa kuongeza mtandao wa bomba kwa kilomita 11 katika mji wa Ruangwa.
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi wa kampuni ya M/STC CONSTRUCTION COMPANY LIMITED Lawrence Nkya alitumia fursa hiyo kumshukuru Serikali ya awamu ya sita kwa hatua ya kuwaamini wakandarasi wa ndani ambapo ameahidi kufanya kazi hiyo kwa weledi na kuukamilisha kwa muda uliopangwa .
0 Comments