Header Ads Widget

HIFADHI YA KATAVI INASIFIKA KUWA NA IDADI KUBWA YA WANYAMA WAKUBWA

  






Na Pamela Mollel,Katavi 


Hifadhi ya Taifa ya Katavi imeanza kuboresha miundombinu ya hifadhi itakayowezesha watalii wa ndani na nje ya nchi wanaotembelea kuweza kuona vivutio kwa ukaribu


Akizungumza na waandishi wa uhifadhi waliotembelea hifadhi hiyo,Mkuu wa hifadhi ya Taifa Katavi,Afisa Uhifadhi Mwandamizi Maneno Peter Maziku alisema lengo la uboreshaji huo ni kuvutia watalii na kuongeza idadi kubwa ya watali, yenye sifa ya kuwa na idadi kubwa ya wanyama kwenye eneo dogo


Alisema kuwa kila aina nne ya wanyama wakubwa ambao ni Simba,Tembo,Chui,Nyati wanapatikana katika hifadhi hiyo isipokuwa Mnyama aina ya faru 


Aliongeza kuwa mbali na wanyama hao hifadhi hiyo inasifika kuwa na idadi kubwa ya wanyama viboko wanaoishi majini katika mto katuma


Aidha Maziku alitaja vivutio vingine kuwa ni pamoja na mti wa mzimu wa katabi ambao makabila yaliyopo karibu na hifadhi hiyo hutumia kufanya matambiko kwa kutatua shida wakiamini kuwa watafanikiwa kutokana na imani zao


"Huu Mti pia unavutia wageni na wanavutiwa kuutembelea kutokana na historia yake"alisema Maziku

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI