Header Ads Widget

BONAZA LA SABINA LIPUKILA CUP 2023 LAFIKIA TAMATI MKOANI RUVUMA.

 


  Na Amon Mtega _Songea.


BONAZA la  Sabina Lipukila Cup 2023 limefikia tamati kwa Timu ya mpira wa Mguu ya Mbinga Road FC pamoja na timu ya mpira wa Pete Njombe Road kutoka Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma  kutwaa ubingwa baada ya  kuwafunga wapinzani wao kwa mkwaju wa penati dhidi ya timu ya Tunduru  Roard FC kisha kujinyakulia kitita cha  pesa taslimu shilingi laki tano , Jezi seti moja  na mipira wa miguu pia zawadi hizo zimetolewa na  kwa mshindi wa mpira wa Pete.


Akifunga mashindano hayo mjumbe wa kamati tendaji Taifa toka  Mkoa wa Ruvuma (KUT) Sabina Lipukila ambaye ndiye mfadhili wa mashindano hayo alisema, lengo la mashindano hayo ni kujenga undugu kwa walimu,kudumusha nidhamu na haiba ya walimu waliyonayo lakini pia michezo inajenga afya kama Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anavyosisitiza watu wafanye mazoezi kwa lengo la kuimalisha Afya zao.



Amesema kuwa bonanza hilo ambalo limefanyika leo Manispaa ya Songea katika viwanja vya shule ya msingi Sokoine ni mwendelezo wa mabonanza mengine ambayo yalishaanza na uzinduzi ulifanyika Novemba mwaka Jana 2022 katika Wilaya ya Mbinga na Namtumbo,na kwamba kupitia michezo hiyo wachezaji watacheza kwa juhudi zote kila mchezaji ameonyesha kipaji chake .


“mimi furahaa yangu kuona mshindi anaposhinda basi anapata motisha kwa hiyo motisha zipo na tutakwenda kutoa zawadi mshindi wa kwanza kuna jezi,mpira wa miguu pamoja na laki 5 alikadharika mshindi wa kwanza kwa mpira wa Pete atapata mpira,jezi na laki tano, lakini wote watakao shika nafasi ya pili kwa mpira wa miguu na Pete watapata jezi na laki tatu .”amesema Sabina Lipukila.



Mchezaji wa mpira wa Pete ambaye timu yao imejinyakulia ushindi wa kitita cha laki tano,jezi na mpira Mwalimu Mery Kapinga amempongeza muandaji wa bonaza hilo  kwa moyo wake wa kujitoa na kuthamini chama cha walimu pamoja na watumishi wake (Walimu) ambapo huku akidai  mashindano hayo kwa ujumla yanaleta hamasa kwa walimu,lakini pia yanawakumbusha kufanya kazi kwa mshikamano kama wafanyakazi .


Kwa upande wake mchezaji wa timu ya Tunduru Roard FC Shukrani  kasim Faraji ambaye alikosa mkwaju wa penati amesema kuwa mashindano hayo yamekuwa chachu kwa walimu lakini pia amepokea matokea japo walikuwa na matumaini ya kuwa washindi lakini kwenye mchezo kuna kushinda na kushindwa au kutoka suluu.



Akisoma taarifa fupi ya bonanza hilo mbele ya mgeni rasmi wa mashindano hayo Afisa maendeleo  ya michezo Manispaa ya Songea Mohamed Kites ambaye ni mchezaji wa timu iliyojinyakulia ushindi ya Mbinga Roard amempongeza bonaza hilo kuwa limekuwa na ushindani  mzuri kutokana na maandalizi yake ikiwemo zawadi kubwa ambazo hazijawahi kutokea kwenye michezo ya bonaza  na  kwamba timu yao itakuwa imeweka historia na watajipanga kwa mwakani ili waweze kutetea kikombe chao.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI