Header Ads Widget

BODI YA WAKURUGENZI MSCL WATAKIWA KUSIMAMIA MRADI WA MELI YA MV MWANZA HAPA KAZI TU KUKAMILIKA KWA WAKATI.

 



NA CHAUSIKU SAID_MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.


Bodi ya wakurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) imetakiwa kuendelea kusimamia mradi wa ujenzi wa meli ya Mv Mwanza hapa kazi tu ili uweze kukamilika ndani ya muda uliopangwa na kuanza kuhudumia Wananchi.


Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete Kwa ya Waziri wa Wizara hiyo Profesa Makame Mbarawa wakati wa hafla ya ushushaji wa meli ya Mv Mwanza hapa kazi tu ndani ya maji katika Bandari ya Mwanza kusini Jijini Mwanza.



Mwakibete ameeleza kuwa serikali imekuwa ikiwekeza kwenye miradi mikubwa ya kinaendelea inayotekelezwa na MSCL Kwa lengo la kuboresha huduma ya usafiri wa abiria na mizigo Kwa njia ya Meli.


"Leo hii tunashudia Meli ikishushwa ndani ya maji kazi nyingi za ujenzi wa meli tayari zimekamilika ikiwa kwenye maji makandarasi anatarajiwa kukamilisha kazi chache zilizobaki na hatimaye Meli ianze kazi" Alisema Mwakibete.


Ameeleza kuwa kujengwa Kwa Meli hiyo kitasaidia kufua masoko mapya ndani na nje ya Nchi Kwa kuanzisha safari mpya zitakazosaidia kurahisisha shughuli za kibiashara.


" Meli hiiitakapokamilika ndani ya mwka huu itasaidia sana katika usafiri na siyo kuongeza idadi ya Meli itatuboreshea usafiri Kwa muda mchache" Alisema Mwakibete.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MSCL Erick Hamis ameeleza kuwa Meli hiyo ikikamilika itahudumia bandari zote kuu za Ziwa Victoria, ikiwemo Bandari ya kemondo, Bukoba, Mwanza, Musoma, portbell,Jinja pamoja na Nchi Jirani ikiwemo Uganda na Kisumu Nchini Kenya.


Hamis ameeleza kuwa Meli hiyo ya Mv Mwanza hapa kazi tu inauwezo wa kubeba abiria 1200 Yani 400 za mizigo na Magari madogo 20 Hadi kukamilika kwake itagharimu sh, Billion 109.


"Wakati serikali ya awamu ya sita inapokea mradi huu ujenzi wake ulikuwa umefika Asilimia 45 lakini mpaka leo Meli inashushwa ndani ya maji imefikia Asilimia 82 na Mkandarasi ameishalipwa Asilimia 88 sawa na Bilioni 93.8" Alisema Hamis.



Ameeleza kuwa Meli hiyo itakuwa na madaraja sita ambayo ni VVIP itakayo kuwa maalumu Kwa viongozi wa Kitaifa ambapo watakuwa wanakaa watu wawili pamoja na Viongozi wa Kitaifa wa Nchi Jirani kama wataruhusiwa kisafiri na Meli hiyo.


Aidha amefafanua kuwa Daraja la mwisho kwenye Meli hiyo litakuwa linabeba abiria 834 na katika Daraja hilo hilo kutakuwa na hadhi ya kisasa na wananchi wataka Kwa starehe na watafanya utalii ndani ya Meli hiyo.



"Ndani ya Meli hii pia kutakuwa na burudani, sehemu za lift, hasa Kwa watu wenye changamoto ya kupanda ngazi ndio wataweza kutumia na wagonjwa pia kutakuwa na zahanati na sehemu maalumu Kwa mama wajawazito" Alisema Hamis.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI