Header Ads Widget

BILIONI 41.7 ZAPITISHWA KUTEKELEZA MIRADI NJOMBE MJI

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Madiwani wa Halmashauri ya mji wa Njombe kwa kauli Moja wamekubaliana kupitisha kiasi Cha zaidi ya  shilingi Bilioni 41.7 ambazo ni rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2023/2024 na kati ya fedha hizo  shilingi bilioni 6.4 ni mapato ya ndani.


Katika kikao maalum cha baraza la madiwani cha kupitisha rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2023/2024 mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Kuruthum Sadick amesema fedha hizo  zinatakiwa kupitishwa  kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa halmashauri hiyo.


Akiwasilisha rasimu hiyo mbele ya baraza maalum la madiwani Afisa mipango wa Halmashauri hiyo Kubeja Ganja amesema mpango huo unazingatia vipaumbele mbalimbali vya Halmashauri pamoja na malengo endelevu ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya elimu ikiwemo shule inayotarajiwa kujengwa katika tarafa ya Njombe mjini.



Wakichangia rasimu hiyo ya bajeti baadhi ya madiwani akiwemo Michael Uhahula,Alatanga Nyagawa na Nickosn Nganyange wamesema wakati wa utekelezaji wa bajeti hiyo Ni muhimu kuzingatia ushauri wa wataalamu ili kuondoa mikanganyiko inayoweza kujitokeza hapo baadaye huku hoja ya ujenzi wa shule ya sekondari tarafa ya Njombe mjini ikionekana kuvuta hisia za madiwani wengi.


Hata hivyo Mwenyekiti wa Halamashauri ya mji wa Njombe Erasto Mpete amesema pamoja na kuwepo kwa ulazima wa kujenga shule hiyo lakini ni lazima majadiliano yenye tija yafanyike ya wapi shule hiyo ya sekondari itajengwa kwa maslahi mapana ya watoto.



Mbunge wa jimbo la Njombe Mjini Deo Mwanyika naye anasema ni lazima eneo la ujenzi wa shule hiyo lifahamike mapema ili fedha ziletwe na zianze ujenzi.


Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amewataka madiwani hao kuacha kuendekeza mijadala ya migogoro ya mtu binafsi na unafiki badala yake wajadili uchumi wa halmashauri na Taifa kwa ujumla.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI