Header Ads Widget

WAZIRI NAPE NNAUYE AZINDUA MNARA WA MAWASILIANO WANGING'OMBE NJOMBE

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema kutokana na kasi ya ukuaji wa teknolojia  hakuna budi serikali ikaendelea kuwekeza kwenye sekta ya mawasiliano kwa kujenga minara ya simu inayoweza kusaidia kupunguza adha kwa wananchi.


Nape ametoa kauli hiyo Wakati akizindua mnara wa simu wa Vodacom katika Kijiji cha Kinenulo kata ya Imalinyi Wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe uliojengwa kwa ushirikiano na serikali kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF na hivyo Ni lazima kuwekaza kwenye mawasiliano ili kuendana na teknolojia hiyo.


Justina  Mashiba  ni mtendaji mkuu wa mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF Ambaye anasema serikali imetoa shilingi bilioni 4.8 kwa ajili ya kujenga Minara 32 katika mkoa wa Njombe ambayo inajengwa kwa ubia wa makampuni ya simu.



Magreth Laurance ni mkuu wa kanda ya nyanda za juu kusini toka kampuni ya Vodacom ambaye anasema mnara huo ulikamilika na kuanza kufanya kazi tangu machi mwaka jana na hivyo umerahisisha huduma ya mawasiliano kwa kiasi kikubwa kwa wananchi wa Wanging'ombe.


Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amesema mfuko wa mawasiliano kwa wote UCSAF umekuwa chachu kubwa ya maendeleo katika mkoa kwani umesaidia kujengwa kwa minara mbalimbali ya mawasiliano.



Upendo Pela Nuru MSIGWA na Philip Mangula ambaye ni makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM Tanzania bara Ni wakazi wa kijiji Cha Kinenulo ambao wameonesha furaha yao baada ya kuanza kupata mawasiliano baada ya kuzinduliwa kwa mnara huo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI