**************************
KATIKA kukabiliana na changamoto ya vifaa vya shule kwa wanafunzi wenye mahitaji Maalum kikundi cha Charity Events na Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere zimesaidia vifaa vya shule kwa wanafunzi hao.
Vifaa hivyo vimetolewa kwa Wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwa Shule ya Msingi Chalinze na Kituo cha Kulea Child Village.
Akizungumza baada ya kukabidhi misaada hiyo ya vifaa vya elimu Naibu Waziri wa Ardhi Ridhiwani Kikwete alisema kuwa Hayati Mwalimu Nyerere kipaumbele alichokiweka ilikuwa ni elimu.
Ridhiwani alisema kuwa vifaa hivyo ni kuenzi maono Nyerere kwani vijana hao wameonyesha uzalendo wa hali ya juu kusaidia watoto wenye ulemavu kwani hiyo ni chachu kwenye sekta ya Elimu nchini.
Naye katibu wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Omary Pumzi alisema kuwa katika kuinua elimu kwa watoto wenye mahitaji Maalum wameungana ili kuwasaidia watoto hao ili waanze masomo wakiwa na vifaa muhimu vya masomo.
Naye Katibu wa kikundi hicho Joseph Moria alisema kuwa pia huwa wanatoa misaada kwa watu wenye uhitaji kipindi cha mfungo wa Kwaresma na mfungo wa Ramadhan ikijulikana kama Furaha Yangu na kusaidia kipindi cha mwisho wa mwaka kwa watoto yatima, wajane na Wazee na wako vijana 140.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze Ramadhan Posi alisema kuwa Shule ya Msingi Chalinze ina wanafunzi mchanganyiko wakiwemo wenye ulemavu 67.
Naye Mwenyekiti wa Kituo Cha Kulea Child Care Village Samwel Kondo alisema kuwa malengo ya kuanzishwa kituo hicho ni kuendeleza ndoto za watoto hao kwa kuwapatia elimu.Baadhi ya vifaa vilivyotolewa ni pamoja na madaftari, kalamu, sare, mabegi na penseli.






0 Comments