Header Ads Widget

UVCCM PICHA YA NDEGE YAWAPATIA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI VIJANA WA KATA HIYO.



**************************

UMOJA wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Picha ya Ndege Wilayani Kibaha imewapatia mafunzo ya ujasiriamali wanachama wake ili wawe na uwezo wa kujitegemea.

Akizungumzia juu ya mafunzo hayo katibu wa UVCCM Kata ya Picha ya Ndege Akothlilian Bake alisema kuwa wameona kuna umuhimu wa kuwapatia ujuzi vijana ili waweze kujipatia kipato.

Bake alisema kuwa wameamua kuunga mkono serikali ya awamu ya sita chini ya Dk Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mafunzo hayo bure kabisa bila ya malipo yoyote.

"Lengo la kutoa mafunzo hayo bure ni kuwahamasisha vijana wetu kwa kuwapa ujuzi ili waweze kujikwamua kiuchumi kupitia ujasiriamali ambapo leo wamejifunza kutengeneza sabuni ya maji na mafuta ya kujipaka,"alisema Bake.

Alisema kuwa wao kama vijana wanamshukuru Rais na wanaona kazi zake kwa vitendo na wamekuwa wakishuhudia jitihada mbalimbali kupitia serikali yake katika kuhakikisha vijana wa nchi hii wanatengenezewa fursa na mazingira wezeshi akiwa na lengo la vijana kifikra na kiuchumi.

Naye katibu wa Wilaya ya Kibaha Mjini Amina Makona alisema kuwa kata hiyo imeonyesha mfano mzuri wa jinsi gani vijana wanapaswa kuwa ili wasiwe tegemezi.

Makona alisema kuwa vijana wanapaswa kuchangamkia fursa za mafunzo kama hayo ili waweze kujikwamua kwani wao ni kundi lenye changamoto nyingi za kiuchumi.

Naye mkufunzi wa mafunzo hayo Mchungaji Brighton Muta alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwani mtu anayejifunza anaweza kutengeneza uchumi wake kwa haraka.

Muta alisema kuwa mafunzo hayo yanamwezesha kijana kujipatia kipato kwa muda mfupi huku akiendelea kupata ujuzi.

Kwa upande wake Thobias Shilole alisema kuwa atajitolea kuwanunulia jezi na mpira ila vijana hao waweze kucheza baada ya shughuli zao kwani michezo ni afya.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI