Na Pamela Mollel,SERENGETI
Hifadhi ya Taifa Serengeti imetembelewa na Spika wa Bunge la India, Mhe. Om Birla ambaye ni mtu maarufu Dunia ikiwa ni sehemu ya mapumziko pamoja na kujionea vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika Hifadhi hiyo iliyojaliwa vivutio lukuki
Akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa ndege wa Seronera mara baada ya mapokezi hayo Naibu Kamshna wa Uhifadhi na Mkuu wa Kanda ya Magharibi TANAPA, Martin Loibooki alisema ujio wa Spika ni fursa kubwa katika kutangaza Hifadhi hiyo maarufu Dunia
Alisema kuwa wao wanajivunia na kuona fahari ujio wa Spika wa Bunge la India pamoja na timu yake itasaidia sanaaa kutangaza Hifadhi
"Spika ni mtu maarufu nani kiongozi mkubwa nchini kwao, ujio wake katika Hifadhi ya Taifa Serengeti utasaidia kuendelea kuitangaza Hifadhi hii na kufanya wageni wengine mashuhuri kutembelea lakini pia watalii kutoka Taifa la India"alisema Loibooki
Kwa upande wake Upendo Massawe, ambaye ni Afisa Mhifadhi Mkuu na Msimamizi wa Idara ya Utalii, Serengeti amebainisha kwamba Hifadhi ya Taifa Serengeti ni kati ya Hifadhi maarufu Dunia na wamejidhatiti katika vilivyo kuhakikisha wageni wote wanaotembelea wanafurahia vivutio vinavyopatikana katika Hifadhi
Hifadhi ya Taifa Serengeti ni ya kwanza kuanzishwa nchini Tanzania iliyojizolea umaarufu zaidi ulimwenguni kwa kutembelewa na wageni mashuhuri Duniani.
0 Comments