Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
WAZIRI wa Kilimo Hussein Bashe amesema kuwa Pembejeo bora za kilimo ikiwemo Mbolea,Mbegu,viwatilifu pamoja na miundombinu sahihi ya umwagiliaji vikitumika vizuri katika kilimo vitasaidia kuongeza tija katika Sekta ya hiyo ya kilimo .
Amebainisha hayo leo Januari 10,2023 jijini Dodoma kwenye Mkutano na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari pamoja,watumishi kutoka katika Sekta ya Kilimo pamoja na wadau wengine wa Sekta ya Kilimo hapa nchini.
Waziri huyo ameeleza katika sekta ya kilimo vitu vinavyohitajika nipamoja na pembejeo bora za kilimo (mbolea,mbegu,viwatilifu) na miundombinu sahihi ya umwagiliaji.
Pia Mheshimiwa Bashe amesema kuwa katika mwaka wa fedha ujao wa 2023/2024 serikali kupitia Wizara ya Kilimo imedhamiria kujenga mabwawa 110 nchi nzima kwa ajili ya kuendelea kuboresha kilimo cha Umwagiliaji.
"Ifikapo Mwaka wa 2030 Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imejiwekea malengo ya kuhakikisha inajitosheleza kwa mahitaji ya Chakula,inaongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo kupitia kilimo cha umwagiliaji kutoka asilimia 10 iliyopo kwa sasa hadi asilimia 50," amesema Waziri Bashe
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt.Stephan Ngailo amesema kuwa ili kupunguza utegemezi wa kuagiza mbolea kutoka nje ya nchi TFRA inaendelea kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vya ndani vya kuzalisha mbolea.
Ngailo ameongeza kuwa kwa sasa asilimia 90 ya mbolea inayotumika nchini inatoka nje wakati asilimia 10 tu ndio inayozalishwa katika viwanda vya ndani.
"TFRA tunaendelea kuhamasisha uwekezaji wa viwanda vya ndani kuongeza uzalishaji wa mbolea na imani yangu ni kwamba itaongezeka kwani kuna viwanda vimeanza uzalishaji wa mbolea ikiwemo kiwanda cha Intracom na Minjingu ambazo pia zimeanza kuuza Mbolea ,"Amesema Dkt.Ngailo








0 Comments