Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi ya chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Fadhili Ngajilo amesema kuwa wataendelea kuendesha mambo yao kwa kasi kubwa ilikuhakikisha kuwa jumuiya ya mkoa wa Iringa inafanya vizuri.
Ngajilo aliyasema hayo jana wakati akifungua warsha ya mafunzo Kwa Viongozi wa jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa iringa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano makao makuu ya Chama cha Mapinduzi mkoani Iringa.
Kwa upande wake MNEC - Wazazi Taifa George Bruno Gandye alisema atahakikisha kuwa vikao na semina za uwezeshaji ndani ya chama vinafanyika mara kwa mara ili kuwezesha kazi zifanyike.
“...Tuna kazi kubwa nyingi za kufanya. Wakati tunafanya kampeni zetu, kati ya mambo mengi ambayo Mwenyekiti na mimi kama MNEC tuliyazungumzia na ninyi kama wajumbe mliyaomba ni pamoja na kuwa na vikao na semina za uwezeshaji. Kazi imeanza semina hii hapa tuweke vichwa shap (makini) tayari kwa kujifunza”
Gandye, akielezea juu ya suala la ukatili wa kijinsia na mmomonyoko wa maadili na kusema kuwa tuna kazi kubwa ya kufanya ili kuilinda jamii na watoto wetu dhidi ya ukatili wa kijinsia.
“..changamoto ambazo mwenyekiti wa vijana amesema ni pamoja na ukatili wa kijinsia na mmomonyoko wa maadili, sasa changamoto hizi inatakiwa tujipange sana kwani tuna kazi kubwa sana kutatia changamoto hizi...”
Pia MNEC Gandye aliwataka viongozi wa jumuiya ya wazazi mkoa wa iringa kuzitumia changamoto zinazojitokeza kama fursa ili ziweze kuwafikisha wanapotaka wao.
0 Comments