Header Ads Widget

MAOFISA ELIMU NA WAKUU WA SHULE RUVUMA WATAKIWA KUPANGA MIKAKATI YA KUONGEZA UFAULU KWA WANAFUNZI.

 




Na Amon Mtega,Matukio DaimaAPP

Ruuvuma

KATIKA kukabiliana na changamoto ya kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari mkoani Ruvuma,maofisa Elimu pamoja na wakuu wa shule wametakiwa kujiwekea mikakati mbalimbali kwa ajili ya kufanya vizuri mwaka 2023 ikiwemo juu ya ufuatiliaji kwa wanafunzi ikiwemo kudhibiti utolo.


Agizo hilo lilitolewa na mwakilishi wa katibu mkuu Tamisemi Dkt.Julius Ningu ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani humo wakati alipokuwa akizungumza kwenye semina elekezi ambapo ilishirikisha maofisa elimu na wakuu wa shule za Msingi na Sekondari toka Wilaya zote za Mkoani hapa uliyofanyika  katika ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari ya wasichana Songea(Songea Girls)Mjini hapa.


Dkt.Ningu pia amewataka wataaluma hao wa elimu kuhakikisha wanafuatilia masuala ya ufundishaji wa wanafunzi shuleni na kufundisha kwa umahili kwa madai kwamba kazi ya ualimu ni wito hivyo wanapaswa kuheshimiwa kwa maelezo kuwa uwezi kupata ushindi kinyume na walimu.


Amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanalinda usalama wa watoto dhidi ya vitendo vya ukatili kwa  vinavyofanywa na watu wasiokuwa na hofu ya Mungu katika jamii.



Naye mkurugenzi Tamisemi Susan Nusu akizungumza kwa niaba ya Naibu katibu mkuu Tamisemi amesema kuwa kutokana na changamoto ya kufeli kwa wanafunzi wa darasa la saba,kidato cha pili na cha nne mkoani humo kila Afisa Elimu kufanya ufuatiliaji shuleni kwa muda wa siku mbili.


Aidha Nusu ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa uanzishwaji wa mashamba ya shule kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa chakula kwa wanafunzi shuleni.


Hata hivyo amewashauri walimu kujenga utamaduni wa kutembelea tovuti ya wizara ya elimu kwa ajili ya kupata miongozo mbalimbali itakayosaidia kuboresha masuala ya elimu hapa Nchini.



Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari Matiri wilayani Mbinga mkoani Ruvuma Lugano Kalunda amesema sababu kubwa iliyosababisha kufeli kwa darasa la sab ana kidato cha nne ni kutokana na masuala ya kimfumo na wazazi kuwa na muamko hafifu katika uchangiaji wa chakula shuleni.



 Pia mkurugenzi Wa Halmashauri ya Songea Vijijini Neema Maghembe ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu ya shule ambayo imewafanya baadhi ya wanafunzi kupenda shule na kuacha tabia za utolo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI