Na Gift Mongi, Moshi
Hodi hodi twaingia uwanjani twajimwaga naomba kuuliza leo kuna nini!Tanzania Tanzania sasa ni furaha hata wenye macho kengefu sasa wayaone!
Sikia watanzania, sikia wanasiasa, sikia msiohusika,hata msiokuwa na mrengo Tanzania kuna jambo lenye matumaini kwa sasa mama kafanya yake!huenda ni maneno yaliyomo kwenye mioyo ya wapenda haki tena walio wengi.
Mama anayetajwa hapa ni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuleta neema ya kufungulia mikutano ya vyama vya siasa ambapo miaka sita nyuma ilikuwa likizo!
Kufunguliwa kwa mikutano ya hadhara sasa kumeenda kuwafikirisha walio wengi jambo linalowafanya kuanza kujipanga upya namna ya kujibu hoja zitakazoelekezwa kwao katika mazingira yakujenga.
Lakini huenda ikawa ni tofauti na inavyodhaniwa hususan wilaya ya Moshi Vijijini ambayo ina mizizi ya kutoka nje ya vyama tawala kwa miaka kadhaa.
Yuvenail Shirima mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Moshi Vijijini anasema kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara ni kama wanaenda kuongezewa nguvu katika siasa.
'Namshukuru rais Dkt Samia kwa kuliona hili sasa sisi kama vijana ambao ndio 'chawa' tunaenda kuongeza nguvu zaidi katika ulingo huu wa kisiasa tena siasa safi na kuijenga nchi yetu'anasema
Anasema anaunga mkono kufunguliwa kwa mikutano hiyo lakini pia ni mwanzo mwingine wakujipanga ili kuleta siasa zenye afya kwa mustakabali wa taifa na sii zile za mapambano.
Mwaka 2020 katika uchaguzi mkuu Grace Kiwelu naye alitupa karata yake kuwania nafasi ya ubunge jimbo la Vunjo kupitia chama cha CHADEMA ambapo kura hazikutosha.
Anasema huu mwaka huenda ukawa ni mzuri kwani kufunguliwa kwa mikutano hiyo 'iliyozikwa'kikatiba kutaenda kuamsha ari kwenye ulingo wa siasa ambazo zilionekana kudumaa kwa kipindi kirefu.
'Tunaenda kufanya siasa safi kuliko wanavyodhani na tulikuwa kifungoni ila maridhiano yamefikia tamati sasa tupo huru katika kuendeleza demokrasia'anasema
0 Comments