Header Ads Widget

JAJI MLACHA ATAKA USULUHISHI UTUMIKE KESI ZA MADAI

 



Na Fadhili Abdallah,Kigoma


MAHAKAMA kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma imewaita wananchi wa mkoa huo kwenye maadhimisho ya wiki ya sheria itakayoanza Jumapili kwenye maeneo

ya viwanja vya Mwanga Centre mkoani Kigoma ili kupata elimu ya kushughulikia mashauri yao ya madai kwa  njia ya usuluhishi na maridhiano badala ya kutumia njia ya hukumu  ya mahakama.


Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma,Lameck Mlacha amesema hayo akizungumza

na waandishi wa habari akielezea kuanza kwa maadhimisho ya  wiki ya sheria yatakayoanza Januari 22 hadi 29 mwaka huu ikiwa ni ishara ya kuanza kwa shughuli za mahakama  kwa mwaka huu.


Ujumbe wa wiki ya sheria kwa mwaka huu unasema Umuhimu wa utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi  katika kukuza uchumi endelevu wajibu wa mahakama na wadau ambapo Jaji Mfaiwdhi alisema kuwa mpango huo unaokoa fedha na muda na kuimarisha mahusiano.


Alisema kuwa kwa kiasi kikubwa kesi za madai zina nafasi kubwa ya kushughukilikiwa kwa njia ya mashauriano na maridhiano badala ya hukumu ya mahakama kutokana na vyanzo vya makosa yenyewe hivyo kwenye wiki hii ya sheria yenye ujumbe usemao tunawhimiza wananchi wajitokeze kupata elimu kuhusu namna ya kushughulikia mashauriano hayo.


Akitoa taarifa kuhusu  mwenendo wa kesi mbalimbali mkoani humo alisema kuwa Mahakama imetekeleza mpango mkakati wa sekta ya mahakama uliowekwa na Jaji Mkuu wa kumaliza kesi kesi katika kipindi kifupi na kwamba kesi zote ambazo zilivuka mwaka 2021 na kuangukia mwaka 2022 zimemalizika.


Kwa upande wake Naibu Msajili wa Mahakama kuu mkoa Kigoma, Gadiel Mariki alisema kuwa mashauri 67 yalivuka mwaka 2021 kwenda mwaka 2022 lakini hadi Desemba mwaka jana mashauri 66 sawa na asilimia 97 yalikuwa yamefanyiwa kazi na shauri lililobaki linaendelea kwa sababu ya rufaa.


Alisema kuwa vikao vya wadau wa kusuka mashauri vilivyokuwa vikifanyika vimekuwa na mchango mkubwa kwenye kumalizika kwa mashauri hayo na kwamba kushauri mashauri mengi kwisha kwenye usuluhishi imechangia jambo hilo.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI