Na Amon Mtega,__Songea
DICKSON NYELELA (46) maarufu kwa jina (KADODA)mkazi wa mtaa wa Shuleyatanga kata ya Shuleyatanga Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma ametoweka Nyumbani kwake katika mazingira ya kutatanisha huku ndugu na majirani wakiomba msaada kwa atakayemuona atoe taarifa.
Akizungumzia tukio hilo ndugu wa Dickson Nyelela ambaye ni Anagret Nyelela amesema kuwa ndugu yao ametoweka Januari mosi mwaka huu akiwa kama anaenda kwenye matembezi ya kawaida ya kuushangilia mwaka mpya cha ajabu hakulejea tena Nyumbani.
Anagret ambaye ni kaka wa Dickson Nyelela amefafanua kuwa ndugu yao anamatatizo ya kutokusikia (Bubu)amekuwa akiishi kwenye Nyumba ya kaka yao kwenye chumba cha nje na kuwa walipoingia chumbani kwake wamekuta begi na nguo zote zipo ndipo walipoamua kutoa taarifa kituo cha polisi cha kidogo kilichopo kituo cha mabasi katika Shuleyatanga na kupatiwa S/TANGA -SO/RB/66/2023 lakini hadi sasa bado hawajafanikiwa kumpata.
Ndugu huyo amefafanua kuwa ndugu yao ni mweupe anaupaa kichwani na anaulemavu wakutokuzungumza yaani bubu na kuwa siku aliyotoweka alivalia nguo za kawaida (Kutokea)kama yupo kwenye matembezi ya kawaida.
Mmoja wa majirani Khashmir Mpangala amesema kuwa baada ya majirani kupatiwa taarifa hiyo wakaanza mikakati ya kumtafuta kwa kuwa kijana huyo hakuwa na shida yeyote na majirani zake zaidi ya kuishi vizuri na kujitolea kufanyakazi za kwake na za kijamii.
Naye mmoja wa wakinamama wa mtaa huo Victoria Kifaru amesema kuwa wamepokea kwa masikitiko juu ya tukio hilo huku wakiomba msaada kwenye Serikali na taasisi mbalimbali ziweze kusaidia juu ya kumpata kijana huyo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Shuleyatanga Paulo Ndunguru amesema kuwa mtaa wake umeshitushwa na jambo hilo na kuwa jitihada za kumtafuta zinaendelea na kuwa kama Serikali ya mtaa huo imewashirikisha na wenyeviti wa mitaa ya jirani kama watapata taarifa ya uwepo wa kijana huyo.
Ndunguru amefafanua kuwa hata kama watamuona kijana huyo katika mazingira ambayo siyo yakawaida watoe taarifa polisi au ofisi ya mtaa kata bila hofu yeyote kwa kuwa mtoa taarifa atakuwa amesaidia kupatikana kwa kijana huyo ambaye amesema hakuwa na tatizo lolote kwenye mtaa huo.
Kufuatia tukio hilo ndugu na majirani wa kijana Dickson Nyelela (KADODA)wameshamtafuta kwenye baadhi ya mapori ya jirani mafanikio hivyo kama kuna mtu atamuona ndugu yao huyo apige Simu Namba -07198-80920/0718-658282.
0 Comments