Header Ads Widget

BODI YA MAJI TANGA YATAKIWA KUIBUA MADUDU TANGA-UWASA

Na Mbaruku Yusuph Matukio Daima APP Tanga.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameiagiza bodi ya maji ya Mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira (tanga-uwasa) kufanya kikao maalum kitakacho washirikisha Wenyeviti wa Serikali za Mitaa,watendaji na Madiwani ili kuweza kubaini changamoto zinazopelekea huduma ya maji kuzorota Jijini hapa.


Kauli hiyo ameitoa katika kikao maalumu kilichohudhuriwa na Maofisa wa Mamlaka ya Tanga-Uwasa,Madiwani na Viongozi wa chama cha mapinduzi baada ya ziara ya Waziri huyo kukagua vyanzo hivyo vya maji.



Waziri huyo alisema ipo haja kwa bodi ya maji kuipitia Mamlaka hiyo kiutendaji na kubaini ubadhirifu unaofanywa ili hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa kila mtumishi atakaebainika anakwamisha utolewaji wa huduma bora ya maji kwa wananchi.


"Labda niwaeleze ukweli kipo kitu hapa na katika kikao hicho cha bodi ya maji nami nitatuma watu wangu na hamta wajua ila nikibaini ubadhirifu wowote sitiwavumilia nitachukua hatua kali"isema Waziri Aweso.


"Tanga-Uwasa jipangeni na kila mmoja wenu awajibike lakini kama hamuwezi kujipanga nitakuja kuwapanga kwa nguvu kama mamlaka inavyoniruhusu kwa mujibu wa sheria"Alisema Mh;Waziri.


Katika hatua nyingr Waziri wa Aweso amemtaka Mkurugenzi wa bonde la Mto Pangani kutokuondoka Mkoani Tanga ili kuhakikisha anakabiliana na uchafuzi wa vyanzo vya maji vilivyopelekea wananchi kukosa maji takriban siku tatu.


Aweso alisema alipokea taarifa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi(ccm)ikimueleza kuwa wananchi Jijini Tanga wapo kwenye taharuki kufuatia kukosekana kwa huduma ya maji Safi kwa siku tatu bila ya taarifa yoyote.


Aidha Waziri Aweso alisema Mkurugenzi wa bonde hilo la Pangani ndio mwenye mamlaka ya kuhakikisha vyanzo vya maji vinatunzwa kwa nyakati zote ili maji yasichafuliwe na kupelekea wananchi kupata maji ambayo si salama.


Alisema kukosekana kwa maji katika maeneo mengi Jijini hapa kumesababishwa na baadhi ya watendaji katika bonde hilo na mamlaka husika kutokuwajiba ipasavyo kitu ambacho kimeleta athari kwa wananchi wengi kukosa huduma hiyo muhimu ya maji.


"Mkurugenzi unatambua kama wewe ndio chanzo cha tatizo hili?nakuomba huna sababu ya kuondoka leo, jipange na timu yako ili kuhakikisha vyanzo vyote vya maji vinatunzwa na vinalindwa ili hali hii isijirudie"Alisema Aweso.


Mkurugenzi wa Bonde la mto Pangani Segure Segure alikiri kutokea kwa changamoto za uchafuzi wa vyanzo vya maji katika eneo la mto zigi na kuahidi kupokea maelekezo ya Waziri mwenye dhamana ili kudhibiti uharibifu huo.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tanga-Uwasa Geofrey Hill alisema uchafuzi wa maji uliofanyika kwa ghafla ulipelekea mamlaka hiyo kufunga maji ili kuanza kuyatibu kabla ya kuleta madhara kwa wananchi.

"Labda niombe radhi kwa kutokutoa taarifa kwa wananchi lakini tulichokifanya baada ya maji kuchafuka kwa kiwango kikubwa tuliamua kuyazuia maji kwenda kwa wananchi ili tuyatibu na kuzuia madhara ambayo labda wananchi wangeyapata"Alisema Hily.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI