Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewahukumu kunyongwa hadi kufa washtakiwa 11 katika kesi ya mauaji ya mwanaharakati wa ujangili, raia wa Afrika Kusini, Wayne Derek Lotter.
Katika hukumu yake iliyosomwa leo Ijumaa, Desemba 2, 2022 na Jaji Laila Mgonya imewatia hatiani washtakiwa hao baada ya kuridhika na ushahidi wa upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake 32 kuwa umethibitisha mashtaka dhidi yao bila kuacha mashaka yoyote.
Waliotiwa hatiani na kuhukumiwa adhabu hiyo ni pamoja na Rahma Almas, mkazi wa Mbagala B, Nduimana Ogiste, maarufu kama mchungaji na raia wa Burundi, Godfrey Salamba mkazi wa Kinondoni Msisiri A na Chambie Juma Ally, mkazi wa Kia/Boma.
Wengine ni Allan Elikana Mafue; Ismail Issah Mohammed (Machipsi); Leornad Phillipo Makoi; Ayoub Selemani Kiholi; Abuu Omary Mkingie na Habonimanda Augustine Nyandwi (pia raia wa Burundi) na Michael Dauv Kwavava;
Lotter ambaye alikuwa Mkurugenzi na Mwanzilishi-mwenza wa Shirika lisilo la kiserikali la PALMS Foundation, lililokuwa linajihusisha na mapambano dhidi ya ujangili.
0 Comments