Header Ads Widget

KAMATI KUU ACT KUINGIA MAFICHONI KUPITIA RIPOTI YA KIKOSI KAZI

 

Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Ado Shaibu (katikati) akitoa maelekezo kwa  viongozi wa chama hicho mkoani Kigoma kuhusu matumizi ya nembo ya ngome ya wazee wakati wa uzinduzi wa nembo ya ngome ya wazee ya chama hicho uzinduzi uliofanyik kitaifa mkoani Kigoma.

(Picha na Fadhili Abdallah).

Mwenyekiti wa Taifa wa ngome ya wazee ya chama cha ACT Wazalendo Yassin Mohamed akizungumza katika uzinduzi wa nembo ya ngome ya wazee ya chama hicho uzinduzi uliofanyika kitaifa mkoani Kigoma.
(Picha na Fadhili Abdallah)
Wazee wa chama cha ACT Wazalendo mkoa Kigoma wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa nembo ya ngome ya wazee uliofanyika mjini Kigoma 
(Picha na Fadhili Abdallah).
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Fadhili Abdallah,kigoma

KAMATI kuu ya chama  Cha ACT Wazalendo inatarajia kukutana hivi karibuni kupitia na kufanya uchambuzi wa kina wa ripoti ya kikosi Kazi cha Kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa nchini na baada ya hapo watatoa msimamo wa chama kuhusu ripoti hiyo na mapendekezo yaliyotolewa.


Katibu Mkuu wa ACT,Ado Shaibu akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa nembo ya ngome ya wazee ya Chama hicho alisema kuwa watapitia neno kwa neno ripoti ya kikosi kazi na mapendekezo yaliyotolewa na baadaye kuona wanakubaliana na lipi na hawakubaliani na lipi na watatoa msimamo wao kwa watanzania.


Shaibu alisema kuwa hata kwa mapendekezo yaliyotolewa na kukubaliana nayo yaliyomo kwenye ripoti hiyo wataitaka serikali kuweka muda wa utekelezaji ili kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa mapendekezo hayo.


 “Haitoshi kusema kuwa mapendekezo yanaitaka serikali kuunda tume huru ya uchaguzi, au kuanza kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ni lazima serikali iwe Commitment (kutoa kauli) kuwa ni lini utekelezaji wa mapendekezo yaliyopitishwa yaanza kutekelezwa,”Alisema Katibu Mkuu wa ACT wazalendo.


Akizungumzia uzinduzi wa nembo ya ngome ya wazee alisema kuwa huo ni mwanzo mpya kwa wazee hao kuona wanabeba jukumu la kusimamia utekelezaji wa mambo mbalimbali yenye faida kwa wazee wote wa Kitanzania na siyo kuishia kuzindua nembo kama alama ya Jumuia hiyo ya wazee lakini iwe kwa niaba ya watanzania.


Alisema kuwa lazima wazee wa chama cha ACT – Wazalendo kusimama kwa niaba ya wazee wa Tanzania kupigania masuala ya msingi yanayowahusu ikiwemo suala la matibabu bure kwa wazee, upatikanaji wa mikopo na ruzuku kwa ajili ya miradi ya kiuchumi kutoka halmashauri kama ilivyo kwa makundi ya wazee na vijana.


Awali akisoma risala kwenye uzinduzi huo Katibu Mwenezi Taifa na mahusiano ya Umma ACT – Wazalendo,Ally Omari alisema kuwa uzinduzi wa nembo ya wazee ni kutaka kutumia nafasi yao kwama wazee kupigania haki na mahitaji mbalimbali ya kibinadamu kwa wazee ambayo utekelezaji wake haifanyiki.


Omari alisema kuwa serikali chini ya Chama Cha Mapinduzi inaeleza mambo mengi kuhusu masuala ya wazee lakini utekelezaji wake haufanyiki na mipango hiyo imeishia kwenye karatasi hivyo wazee wa ACT wazalendo wanataka kusimamia jambo hilo kuona serikali inasimamia kwa vitengo mambo yanayoahidiwa kutekelezwa kwa wazee.


Mwenyekiti wa Ngome ya Wazee Taifa, Yassin Mohamed akizungumza katika mkutano huo alisema kuwa bado utekelezaji wa masuala mengi kwa wazee hayafanyiki na haya yameshuhudiwa maeneo mbalimbali ikiwemo kwenye upatikanaji wa huduma za matibabu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI