Header Ads Widget

WADAU WA BAHARI NCHI 15 ZA AFRIKA WAKUTANA DAR KUJADILI NAMNA BORA YA KUTUNZA MAZINGIRA YA BAHARI

Na fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam

Imeelezwa kuwa Ili kuhakikisha mazingira ya Bahari na maji yanatuzwa wadau wa mazingira kutoka nchi wanachama 15 wa Afrika wameshiriki katika warsha ya siku tatu kwa ajili ya kukuza uelewa wa pamoja juu ya mkataba wa kimataifa wa Utunzaji wa Mazingira ya Bahari.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya uchukuzi) Dkt. Ally Possi amesema kuwa Mwitikio wa nchi mwanachama umekuwa mkubwa na ni jambo ambalo dunia imeanza kuipa kipaumbele mkataba wa kimataifa kwa ajili ya kulinda mazingira ya bahari ili kuhakikisha viumbe vitakavyozaliwa majini vinakuwa hai.


Amesema kuwa, hali ya bahari kwa sasa  mazingira ni mazuri lakini tahadhari mbalimbali lazima zitolewa kwa ajili ya Vizazi vya vijavyo, kwani endapo maji yaliyokaa muda mrefu kwenye meli yatashushwa yanaweza kuzalishia viumbe wengine hatarishi na kupelekea kutofikia uchumi wa bluu .


"Ifahamike kuwa vyanzo vya maji hususani bahari vinasimamia sera ya uchumi wa bluu, sasa bahari inapochafuka au inapoharibiwa kimazingira, sera ya uchumi wa bluu inakuwa ngumu kufikiwa kwani viumbe ambavyo vinafanyika kuwa uchumi vitapotea pamoja na vyombo vya usafiri majini vitaharibika na kushindwa kufanya kazi inayotakiwa."amesema Dkt. Possi


Ameongeza kuwa, mkutano huo utatilia mkazo wa uridhiaji wa itifaki ya sheria ya bahari kwaajili ya kuendeleza uelewa mpana wa wadau wote.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Kaimu Abdi Mkeyenge amesema Shirika hilo limekasimiwa mamlaka ya kudhibiti mazingira ya majini na maji yanayotokana na uchafunzi wa vyombo vya usafiri majini hivyo madhumuni ya warsha hiyo ni uelewa wa pamoja wa Jinsi ya kudhibiti maji, kusimamia masuala ya usafiri majini.


"Kwa kukaa sana yale maji inawezekana kuna viumbe ambavyo vinazaliwa na yale maji yaliyokuwa kwenye meli yakimwagwa baharini katika maji ya kitaifa au eneo lolote la bahari kuna uwezekano wa kushushwa na viumbe wengine ambao wamezaliwa baada ya yale maji kukaa muda mrefu,kwenye Meli"amesema.


Amesema uchumi wa bluu unaweza usifikiwe kama maji yanakuwa hayadhibitiwi, hivyo, uchumi wa bluu hautofikiwa kama mikataba hiyo haitoridhiwa na kuzingatiwa ni jinsi gani wanaweza kujikinga na hivyo viumbe ambavyo vinaweza kuzalishwa.


Ameongeza kuwa Shirika la Kimataifa la Bahari linatoa elimu kwa Taasisi mbalimbali zinazohusika na masuala ya usafiri kwa njia ya maji, taasisi zinazohusika na masuala ya bahari zimeshiriki warsha hiyo ili kuwa na uelewa wa pamoja ili mkataba utakaporidhiwa na kutengeneza kanuni za Kutumika hapa nchini.

Naye, Mkurugenzi wa Usalama na Mazingira Baharini kutoka Wizara ya Ujenzi na uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi, Stela Katondo amesema kuwa maji yanayobebwa na meli yanasaidia meli pale ambapo inakuwa haina mzigo au ikiwa na mzigo mdogo, yanapunguzwa au kuongezwa ili kuweka uzito sawa katika meli na maji hayo watu wenye meli wamekuwa wakiyamwaga baharini jambo ambalo sio zuri.


"Maji hayo yanaviumbe na mimea ambayo sio asili ya huku kwetu kwa hiyo ikitokea yanamwagwa baharini yatakuwa na viumbe wavamizi ambao wataleta namna tofauti ya kimazingira hivyo, IMO inaona umuhimu wa kuweza kudhibiti hali hiyo kwa sababu kimazingira sio sawa,"amesema 

Ameongeza kuwa, "kinachotakiwa ni kutomwaga baharini kama nchi mwanachama wa IMO, tunatakiwa kuridhia mkataba huo ili kuweza kusimamia kuwa haitakiwi ukifika bandarini kumwaga maji inatakiwa kwenda kumwaga katikati ya bahari ili yasiweze kuleta shida katika eneo letu la mazingira ya maji"


Amesema kwa Tanzania Sasa hivi wapo katika hali nzuri kwa sababu wameshaanza kuridhia mkataba pia amesema kama wizara wameshatoa maoni na mapendekezo kwa wadau mbalimbali wanaohusika na mkataba huu, ambapo wameanza kupokea maoni ya wadau.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS