Header Ads Widget

UMASIKINI, VITENDO VYA UDHALILISHAJI NA UKATILI WA KIJINSIA VYACHANGIA ONGEZEKO LA USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU

 

Picha na Maktaba


NA THABIT MADAI, ZANZIBAR –MATUKIO DAIMA 


SI Ajabu tena kusikia neno Usafirishaji Haramu wa binadamu hapa Nchini ukiwa na maana kuwa, ni Usafirishaji wa Watu kwa njia ya nguvu, tishio, Kulazimishwa, Udanganyifu au utekaji nyara kwa lengo la dhulma.


Dhana nzima ya Usafirishaji haramu wa Binadamu ni pana huku Tanzania ikitajwa kuwa  miongoni mwa nchi zenye matukio ya usafirishaji haramu wa binadamu, hasa kwa upande wa watoto wenye ulemavu na wasichana.


Takwimu halisi za Watu waliokumbwa  matendo hayo ya Usafirishaji haramu wa binadamu bado imekuwa kizungumkuti kutokana na Mamlaka hazina takwimu halisi licha ya Vijana wa Kike na Kiume nchini kukumbwa na kadhia hiyo  ambayo inaelezwa kuwa ni tishio  Ulimwenguni kote.


Wanaharakati, Serikali pamoja na Mashirika yasiyo ya Kiserikali wanaeleza sababu mbalimbali zinazopelekea  kushamiri kwa Usafirishaji haramu wa Binadamu huku umasikini ukielezwa kuwa ni moja ya Sababu inayopelekea kuchochea kwa kadhia  hiyo.


*SABABU*

Ahmad Mwendadi Afisa Mwandamizi kutoka Sektarieti ya kuzuia na Kupambana na Usafirishaji wa Binadamu alisema kuwa, Umasikini katika jamii ni nyenzo inayopelekea kuwepo kwa Usafirishaji Haramu wa Binadamu ambapo Vijana wengi wanashawishiwa kutokana na Umasikini wao kujikuta wanaingia katika kadhia hiyo.


Picha na Maktaba


“Umasikini husababisha Vijana wa Kike na kiume kushawishiwa kuwa kuna Ajira Nnje ya Nchi na Mwishoe wanapofika katika hizo Nchi vijana hao kuanguka katika Kazi za Madanguro ambapo hutumikishwa kingono,” Alieleza.


Aliongeza kuwa wamepokea wahanga wengi wa kadhia hiyo ambapo walipowahoji juu sababu iliyopelekea kuingia ni Umasikini wao uliokithiri.


Aidha alieleza kuwa, Kukithiri kwa  Vitendo vya Udhalilishaji na Ukatili wa Kijinsia navyo husababisha kuwepo kwa Matendo na biashara ya Ushafirishaji haramu wa binadamu ambapo Vijana wengi hususani wa Kike hujikuta wanaingia mikononi mwa Maharamia na kukimbia aibu iliyowatokea mara baada ya kufanyiwa kwa vitendo vya Udhalilishaji na Ukatili wa Kijinsia.


“Udhalilishaji na Ukatili wa Kijinsia katika jamii hupelekea kwa kiasi kikubwa sana Vijana kuingia katika Kadhia ya Uafirishaji haramu baada Vijana hukimbia katika Maeneo yao kutokana na alifanyiwa Vitendo vya Udhalilishaji na Ukatili au anakimbia katika Maeneo hayo ili asifanyiwe vitendo hivyo na baadae kuangukia katika Mtandao huu,” Alieleza.


Alifafanua kuwa ndoa za kulazimishwa huwa ni miongoni mwa sababu zinazopelekea kukithiri kwa biashara ya Haramu ya Binadamu.


“Lakini pia elimu duni pamoja na kutokujua haki za watoto hupelekea watoto wengi kutumikishwa kwa maslah ya watu wengine,”aliongeza Kufafanua.


Hata hivyo aliongeza kuwa, tafiti mbalimbali zimeonesha kuwa vyanzo vikubwa vya vitendo vya utumikishwaji watoto katika shughuli za kijamii na kiuchumi ni ukosefu wa elimu ya kujua haki za watoto na umaskini uliokithiri.


Nae Adwin Migambila akizungumza na Waandishi wa habari huko maru maru alieleza kwamba, kusambaratika kwa familia nyingi katika jamii huwa ni chanjo cha Vijana wengi kukumbwa katika kadhia ya Usafirishaji haramu wa Binadamu pamoja na watoto wengi kutumikishwa kinyume na shaeria.


Alieleza, ndoto za Vijana wengi kufika katika Maeneo ya Mjini huwa chanjo cha kushamiri kwa biashara hii ya Usafirishaji haramu wa Binadamu ambapo Vijana wengi wa Kike  na Kiume katika maeneo ya Shamba huwa na ndoto za kufika katika mjini kwa lengo la kutafuta Maisha.


“Vijana wengi wa Kike na hata wakiume huwa na ndoto za kufika katika maeneo ya mijini kwa lengo la kujikwamua kimaisha ambapo sababu hiyo hupelekea kushawishika kwa urahisi na wale wenye mtandao wa Usafirshaji binadamu,” aliongeza.


Hata hivyo alibainisha kwamba chanjo kikuu ni Umasikini uliokithiri na kupelekea Watoto kutumikishwa pamoja na Wasichana wengi kusafirishwa nnje ya Nchi kwa ajili ya kuahidiwa kutafutiwa kazi zenye Maslah makubwa.


“Vijana wengi wanaposafirishwa na kwenda Nnje ya Nchi kazi wanazokutana nazo huwa ni kinyume na zile ambazo walioahidiwa au wakikutana na kazi zile walizoambiwa basi maslah yanakuwa tofauti na makubaliano waliokubaliana,” alibainisha.

Picha na Maktaba


“Kadhia hii ni kubwa sana, Vijana na Watoto huathira sana hivyo tunapaswa kwa pamoja kuungana na kukabiliana nayo,”


*NINI KIFANYIKE*

Nae Sharifa Hamad Makame Afisa Msimazi na Ufuatiliaji wa Kuzuia na Usafirishaji Haramu wa Binadamu katika Bandari ya Malindi alisema Elimu inahitajika katika jamii ili kuodoa kadhia hii ambayo kwa sasa imekuwa ni janga kubwa.


“Kwanza jamii inatakiwa ielimishwe juu ya suala la Usafirishaji haramu wa Binadamu maana jamii yetu bado haina uwelewa wa matendo haya, Mfano hapa bandarini tunapata Watoto ambao ni wadogo wanasafirishwa kutoka maeneo ya Bara na kuletwa Unguja kwa ajili ya kuja kufanyishwa kazi za ndani ambapo wengine wanabakwa,” Alieleza.


Aliongeza kuwa Watoto, Wazazi pamoja na Mawakala hawana uelewa wa kutosha juu ya Matendo haya ambayo ni haramu na kinyume na Sharia na Kanuni za Nchi.


“Haya matatizo ni mengi sana hivyo Wazazi, Walezi, maafisa na wadau mbalimbali kuhakikisha wanatoa Elimu usafirishaji haramu wa binadamu halipo ndani na NMnje ya Nchi ambapo vijana wengi wanaathirika,” Alisema.


Aidha Alisema kuwa juhudi mbalimbali zinahitajika katika kuhakikisha Sheria iliyopishwa juu ya Usafirishaji haramu wa Binadamu inaeleweka na kutumika kwa maafisa mbalimbali wanaoshughulikia suala hilo.


“Kwaiyo tuhakikishe sheria inaeleweka kwa maafisa na Wasimamizi wa kuzuia Usafirishaji haramu wa Binadamu pamoja na kwa jamii nzima waifahamu na kuielewa tutasaidia katika kuzuia na kupambana nalo,” Alieleza.


Kwa Upande wake Jema Mdemu Afisa Mradi kutoka taasisi ya C-SEMA alisema kwamba Mashirkiano kwa wadau mbalimbali yanahitajika katika kuhakiksha Suala la Usafirishaji haramu wa Binadamu linazuilika na kupunguza athari kwa jamii.


Alisema,  Mashirikiano ya Pamoja kwa wadau mbalimbali yanahitajika ili kuweza kukabiliana na tatizo hilo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI