Header Ads Widget

WANAHABARI IRINGA WAHAMASISHA UCHANGIAJI DAMU HOSIPITALI YA RUFAA YA MKOA WA IRINGA

 



Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa ikishirikiana na waandishi wahabari mkoani hamo, wameanzisha kampeni ya utoaji elimu kwa wananchi juu ya uchangiaji damu ili kuepukana na uhaba wa damu salama unayo ikabili hospitali hiyo kwa hivi sasa.

Akielezea kampeni hiyo mganga mfawidhi wa hospital ya rufaa mkoa wa Iringa Daktari, Alfred Laison Mwakalebela amesema kampeni hiyo  itakwenda sambamba na uzinduzi wa uchangiaji damu tarehe 1,1,2023 ikiwa ni siku ya kwanza ya mwaka mpya, uku  zoezi hili likiwa na kauli mbiu ya inayosema “zawadi ya mwaka mpya  kwa wananchi wa Iringa katika kuboresha afya watu wasiishiwe na damu na wasipate madhara kutokana na upungufu wa damu”.

Dkt, Mwakalebela amesema mkoa wa Iringa kwa ujumla unatumia chupa za damu salama mia sita kwa mwezi uku tegemeo kubwa likiwa ni wanafunzi wa shule za sekondari na kipindi shule zikifungwa mkoa huo unakabiliwa na upungufu wa damu salama.

Amewataka viongozi mbalimbali katika ngazi zote  kuwahamasisha wa wananchi wao kuwa na tabia ya kujitolea damu ili kuweza kuokoa Maisha ya watanzania wengine, “Nipende kuwahamasisha wananchi wa mkoa wa Iringa, taasisi mbalimbali zihamasishe watumishi wake, viongozi wa bodaboda kwa pamoja waungane pamoja na viongozi wa dini kuwahamasisha waumini wao kila wanapokuwa ibadani ili kuwezesha tabia ya uchangiaji damu”.

Kwa upande wake, muuguzi mkuu mkoa wa Iringa Mosses Kawete, amesema mkoa huo umejipanga vizuri kwa kushirikiana na wakurugenzi wa  halmashauri zote za mkoa huo kwa kutoa muongozo ambao utapeleke zoezi hilo kuwa endelevu ili kuondokana na upungufu unatokea mara kwa mara katika mkoa huo uku akiitaja Halmashauri ya mji wa Mafinga kuwa kinara katika uchangiaji wa damu katika mkoa wa Iringa.

Naye mwakilishi wa wanahabari mkoa wa Iringa, Silvanus Kigomba ameelezea sababu zilizopelekea kuunga na hospitali ya rufaa ya Iringa katika kuanda kampeni hiyo ya kuhamasisha uchangiaji damu kwa wananchi wa ili kuweza kuwaokoa wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo wakihitaji damu, pamoja na kuelezea utaratibu wa kutembela taasisi mbalimbali pamoja nanyumba za ibada ili kuwahamasisha waumini kujitokeza katika zoezi hilo ambalo uzinduzi wake ni tarehe 1,1,2023.

“Tumeanda utaratibu mbalimbali wa kuwatembelea wananchi ikiwemo kuandika barua ambazo zipelekwa katika nyumba zote za ibada katika ili kila muumini na dini yake apate taarifa hii na kuweza kujitokeza kwani zoezi hili ni endelevu hivyo tutakuwa tunakumbushana mara kwa mara”

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI