Header Ads Widget

TASAF KWA KUSHIRIKIANA NA UNICEF YASAIDIA VIFAA KWA WASICHANA.

MFUKO wa Maendeleo ya Jamii Nchini (TASAF) Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na Shirika la kusaidia watoto Duniani (UNICEF) umetoa msaada wa vifaa vya usafi 16,754 kwa watoto wa kike waliobalehe waliopo kwenye mfuko huo.


Hayo yalisemwa na Mratibu wa Tasaf Mkoa wa Pwani Roselyn Kimaro alisema kuwa lengo ni kufikia wasichana balehe  16,754 ambapo hadi sasa wameshagawiwa 11,350 na zoezi linaendelea. Vifaa hivyo ni kwa ajili ya usafi ikiwemo sabuni ,ndoo pamoja na taulo za kike.


Kimaro alisema kuwa walengwa hao kutumia vizuri misaada wanayopewa  ili kuwasaidia na kuwataka wazazi kuzungumza na watoto wao hasa kipindi wanachobalehe kwa Lengo la kuwa wasafi,kujiepusha na mimba za utotoni na magonjwa ya zinaa.


Naye Mratibu wa Tasaf Chalinze Flora Godfrey Barakana alishukuru kwa watoto kupata msaada huo . Alisema lengo la msaada huo ni kumsaidia mtoto wa kike  awe huru hasa katika kipindi cha kupata hedhi yake ya mwezi.


Kwa upande wake Anita Philemon mratibu wa Tasaf Kibaha Mjini alisema vifaa hivyo vitasaidia watoto hao kwa Maendeleo yao shuleni na watapewa mafunzo ya namna ya kutumia kabla ya kuvitumia na kuwaomba taulo za kike ni kwa ajili ya msichana mmoja mmoja na sio vya kuazimana ili kulinda afya zao.


Naye mnufaika wa Tasaf ,Sadi Athumani alieleza elimu waliyoipata wataenda kuifanyia kazi na kuwa mabalozi kwa wengine kuwafundisha kujenga tabia ya usafi na kujilinda na vishawishi ili kuendelea na masomo kutimiza ndoto yao .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI