Header Ads Widget

SMILE WATOA ELIMU YA HEDHI SALAMA




Mratibu wa miradi wa shirika lisilo la kiserikali la  Smile for Community Aneth Kiyao amewataka wakazi wa kijiji cha Ndumbwe kuliona suala la hedhi kwa watoto wa kike ni suala la kushirikishana ili kuweza kumsaidia motto wa kike na kumpa nguvu ya kusema pale anapopatwa na changamoto.


Kauli hiyo ameitoa wakati akizugnumza na wananchi wa kijiji cha ndumwe halmashauri ya mtwara vijijini katika mkutano na wanakijiji ambapo alisema kuwa shirika hilo linafanyakazi kwa ufadhili wa Legal Services Facility kwa mradi wa haki ya afya kwakusaidia jamii katika masuala ya afya, mazingira, elimu na  hedhi salamaa.


“Haki ya afya kutoa msaada kwa watoa msaada wa kisheria ambapo utawasaidia mabinti na vijana kupata msaada wa kisheria na kugawa sodo kwa watoto waliopo shuleni”



“Kujenga uelewa juu ya masuala ya balehe na kupinga ukatili kwa vijana na kuelimisha wanajamii kwakuwa wengi hawawajui kama kuna watoa msaaada wa kisheria wakidhani kuwa kazi yao ni mirathi ama talaka tunafanya mikutano ya hadhara na kuwaelewesha”


“Ubakaji mimba za utotoni kwakuwa wanaowapa ujauzito watoto wanamalizana majumbani tunatengeneza jamii ambayo sio salama tunawajengea uwezo ili waweze kujua haki zao na kama wanashida yoyote inayohitaji msaada wa kisheria waende wapi”



Bernadetha Majivuno msaidizi wa kisheria Kata ya Kitere alisema kuwa uelewa mdogo unakwamisha utoaji wa elimu ya masuala ya kisheria kwa wananchi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI