TANDAHIMBA
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanal Patric Sawala amelipongeza Shirika lisilo la kiserikali la Search for Common Ground ambalo limetoa kofia ngumu 30 kwa waendesha Pikipiki wa Wilaya hiyo.
Akikabidhi pikipiki hizo kwwa waendesha madereva hao alisema kuwa wamepata kofia hizo ili kuwaweka katika usalama zaidi wamapopatwa na matatizo mbalimbali ikiwemo ajali ili waweze kunusurika.
Alisema kuwa mbali na hakikisha kuwa wanapata kofia ngumu lakini niwaase nimuhimu kuwa na bima, lesseni na kofia ngumu.
“Sio jambo gumu kuwa rafiki wa Polisi hautamkimbia kwakuwa unatii sheria bila utii kwa msaada huu sitegemei kuona mwendesha pikipiki akipita barabarabi bila kuvaa kofia ngumu natoa rai kwa Jeshi la polisi ili kuhakikisha kila mmoja anavaa kofia ngumu akiwa anaendesha pikipiki”
Nae Mkuu wa usalama barabarani Wilaya ya Tandahimba ASP Dickson Kachila alisema kuwa tunatoa elimu ya mara kwa mara kwa waendesha pikipiki ili waweze kufahamu umuhimu wa kuvaa kofia ngumu, kuwa na bima na kuwa lesseni.
"Tumepokea helmet 30 kwa kila wilaya ambazo ni mwanzo tu hili litakuwa ni zoezi endelevu takwimu za ajali za barabarabi ni nyingi hivyo wadau wanalazimika kuisaidia serikali Uendeshaji wa vyombo vya moto unaendana na sheria za usalama barabarani kila mmoja anatakiwa vae anapokuwa kwenye pikipiki"
“Usafi wa mwili ni muhimu oga vaa vizuri viatu vya kufunika na usisahamu kuvaa kofia ngumu ili kuepusha na majanga mbalimbali hasa unapopata ajali” alisema Kachila
Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tandahimba ambaye pia ni Oparesheni ofisa wilaya ASP Moremi Maheri alisema kuwa uvaaji wa kofia ngumu unapunguza migogoro kati ya Askari wa usalama barabarani na watumiaji wa barabara hasa waendesha pikipiki.
“Ipo migogoro kati ya boda na trafik ambao hutokana na kutokuwa na helmet wao wakaona vema kutuletea hii kwetu ni moja ya maboresho muhimu lengo kuu ni kuhakikisha kuwa zinatumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa na kupunguza migogoro hiyo”
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Baisa Baisa alisema kuwa tunafahamu umuhimu wa kuvaa kofia ngumu hasa unapoendesha pikipiki ambapo inazuia kichwa na kuzuia makosa mengine uliyonanayo pia unapokamatwa
0 Comments