NA CHAUSIKU SAID,
MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.
Mwenyekiti Mpya wa chama Cha mapinduzi Mkoani Mwanza Sixbert Reuben amewataka viongozi waliochaguliwa kuanzia ngazi ya Matawi, Mashina na kata kuhakikisha wanawatumikia wananchi na kuachana na tabia ya kupandisha mabega na kujiona miamba Kwa vyeo vidogo vidogo walivyovipa.
Maagizo Hayo ameyatoa wakati wa hafla fupi ya mapokezi iliyofanyika Mkoani hapa na kueleza kuwa Kila kiongozi anapaswa kuwa nyenyekevu na kuwatumikia wananchi.
Reuben ameeleza kuwa wakifanya kazi Kwa umoja na ushirikiano hakuna mtu atakayeweza kukitingisha na kukiangusha chama hicho.
" Mzee mmoja aliniambia kuwa Ccm ni Kama pori la miti, pori like la miti kama usipotokea mtu ndani yake na uakasaliti miti mingine pori litabaki salama na sisi Wana Ccm tukiwa hivyo chama cheti litabaki kuwa salama" Alisema Reuben.
Aidha ameeleza kuwa serikali ya awamu ya sita ilipoingia madarakani Nchi nyingi za Afrika na Ulaya zilikuwa zimekubwa na janga la Uviko 19 pamoja na vita Ukraine na Urusi hivyo kupelekea Nchi hizo kukubwa na mfumko wa Bei na sio Tanzania peke yake.
"Uzalishaji mwingi na usafirishaji unahusisha mafuta hivyo Nchi nyingi zilikuwa na mfumko wa bei kutokana na vita kutoka Nchi za wenzetu" Alisema Reuben.
Amesema kuwa pamoja na misukosuko yote iliyotokea bado Tanzania imebaki salama na mpaka sasa hakuna mradi ambao unalegalega na hakuna mradi unaosubili Kupewa pesa yote inakwenda kama ilivyopangwa.
Kwa upande mwingine ameyataka makundi ya machinga na Bodaboda kumpa muda ili aweze kukutana nao ili kuona namna ya kuweza kutatua changamoto zao zinazowakabili.
Baadhi ya viongozi waliochaguliwa wamempongeza Mwenyekiti Kwa ushindi mkubwa alioupata na kumuahidi watahakikisha wanampa ushirikiano ili waweze kukisongesha chama mbele Kwa masilahi mapana ya Nchi na chama chenyewe.
"Tutahakikisha tunatoka ushirikiano Kwa Mwenyekiti wetu ili tuweze kusonga mbele Kwa kuleta Maendeleo ndani ya chama chetu" Walisema.
0 Comments