Header Ads Widget

RC MAKALLA: RAIS DKT. SAMIA AMEIDHINISHA BILIONI 4 KUJENGA MADARASA 207 WILAYA YA TEMEKE.

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo ameendelea na ziara ya ukaguzi Maendeleo ya Ujenzi wa vyumba vya Madarasa Mkoa huo, na Leo ilikuwa zamu ya Wilaya ya Temeke ambapo ameelekeza Halmashauri hiyo kuhakikisha Madarasa yanakamilika kabla ya Disemba 30 mwaka huu.


RC Makalla amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maamuzi sahihi ya kutoa fedha ili kuhakikisha kila Mwanafunzi anasoma kwenye mazingira Bora na kuwaondolea Wazazi usumbufu wa michango Kama miaka ya nyuma.


Aidha RC Makalla ameshuhudia Ujenzi wa Madarasa ukiendelea vizuri ambapo Wilaya ya Temeke ilipokea Shilingi Bilioni 4.1 kwa ajili ya Ujenzi wa Madarasa 207 ikiwemo ya Gorofa na Mtawanyiko ambapo mpaka Sasa Madarasa 97 yapo kwenye ngazi ya Ujenzi wa Msingi, 32 ukuta, 67 Yanaezekwa na 11 Ujenzi unaanza kesho Baada ya kupatikana kwa maeneo.


RC Makalla pia amepokea taarifa ya Wilaya juu ya idadi ya wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na masomo mwezi Januari mwakani ambapo Kwa Shule za Awali wanaotarajiwa ni wanafunzi 6,343, Msingi wanafunzi 26,000 na Sekondari 23,000.


Ifahamike kuwa Mkoa wa Dar es salaam ulipokea zaidi ya Shilingi Bilioni 12.3 kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vya Madarasa kwa ajili ya wanafunzi wa Shule za Awali, Msingi na Sekondari ambapo pia amesisitiza Ubora wa Majengo yatakayojengwa.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI