Na Mbaruku Yusuph Matukio Daima APP Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hasan ametoa zawadi ya Sikukuu ya Christmas na Mwaka mpya yenye thamani ya zaidi ya Shs Mil 11 kwenye vituo 13 vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu na vituo 2 vya Wazee wasio jiweza Mkoani Tanga.
Akizungumza katika utoaji wa zawadi hizo kwa niaba ya Rais Mkuu wa Mkoa Tanga Omary Mgumba alisema Rais ameguswa na maisha ya watoto hao katika vituo hivyo sambamba na wazee ambapo awali waliishi katika mazingira hatarishi zaidi.
Aidha alisema msaada wa chakula na mahitaji mengine ya kibinaadamu yaliyotolewa na Rais yanakwenda kuwanufaisha watoto 388 na wazee 36 kwa Mkoa mzima hasa katika kipindi hiki cha Siku Kuu na Mwaka mpya.
Alisema kwa kuona umuhimu wa makundi hayo Serikali inashirikiana na wadau mbali mbali kuhakikisha inafikisha huduma za kijamii ikiwemo vyakula,malazi,matibabu ili kuweza kupunguza kama si kumaliza idadi ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Kwa upande wake msimamizi wa kituo cha Nyumba ya furaha kilichopo Jijini Tanga Consolata Aloyce alesma wapo watoto 70 ambao wanapatiwa huduma ya kulelewa katika kituo hicho sambamba na Masister 12 na wamama 2 ambao wanamajuku ya kutunza watoto hao kwa maadili ya Kitanzania.
"Tunaishi na watoto hawa na kufuata taratibu za Serikali kupitia ofisi ya ustawi wa jamii na ili kukidhi taratibu za kuwapata hapa kwa sasa tunae mtoto mdogo kabisa ambae anaumri wa miezi sita na anaendelea vizuri"Alisema Aloyce.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa ambae pia ni Mwenyekiti kamati ya Ulinzi na usalama ya Mkoa alitoa rai wakati huu wa kuelekea sikukuu ya Christmas na Mwaka mpyawananchi washeherekee bila ya kuvunja sheria na kutokufanya vurugu ya aina yoyote.








0 Comments