Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara Shadida Ndile ameshamasisha mpira wa miguu Kwa wanawake kwakushiriki katika mechi ya KIRAFIKI kati ya Tari Naliendele Queens iliyopo chini ya Taasisi ya Utafiti wa kilimo Tanzania TARI kituo cha Naliendele na Timu ya Snake Queens ya Namichiga Wilayani Ruangwa ambapo Timu ya Tari Naliendele Queens walishinda Goli nne (4) kwa tatu (3) mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Majaliwa.
Ndile amesema mchezo huo umesaidia kujenga mahusiano mazuri kwa Wachezaji hao Pamoja na kutangaza Kilimo kwa kuwa wapo Wananchi wanaotoka Manispaa ya Mtwara Mikindani na kwenda Wilayani Ruangwa kwa ajili ya shughuli za Kilimo na ndio maana wakafuatana na Wataalam wa Kilimo kutoka kituo cha Tari Naliendele ili kuwapa Elimu Wananchi wa Ruangwa juu ya mambo mbalimbali yanayohusu Kilimo.
Kwa upande wake Mratibu wa Uhaulishaji wa Teknolojia na Mahusiano Tari Naliendele Bakari Kidunda ambae ni amewashukuru Viongozi wa Wilaya ya Mtwara kwa kuwaunganisha na watu wa Ruangwa ili kufanikisha Tamasha hilo.
Hata hivyo amesema popote wanakuwa na Wataalam wanaotoa ushauri wa maswala ya Kilimo na pia wanauza Mbegu bora za mazao mbalimbali.
Nae Mratibu wa zao la Karanga kitaifa ambaye pia ni mtafiti wa zao hilo Dokta Happy Daudi amewataka Wananchi kuchangamkia fursa kwenye Kilimo kwa kuwa Msimu wa Kilimo umefika na kuwashauri wakulima walime Kilimo chenye tija kama vile kulima kwa nafasi kwa kuwa Kilimo ni biashara.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Andrew Chikongwe amemshukuru Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Shadida Ndile kwa kuongoza Timu hiyo kwenda Ruangwa kwa kuwa imewasaidia kujenga Mahusiano huku akitoa wito kwa Wananchi wa Ruangwa kupanda mbegu badala ya Nafaka.
Taasisi hiyo imejiwekea utaratibu wa kutoa elimu kwakutumia michezo kwa kuhaurisha tekenologia zetu ambazo zinafanyiwa utafiti na Taasisi yetu Ili kufikisha Teknolojia Kwa wananchi Kwa urahisi Zaidi.









0 Comments