RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi za vyakula kwa Makao ya Malezi ya Watoto vituo 37 vilivyopo Mkoani Pwani kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Christmas na mwaka mpya.
Aidha vyakula vilivyotolewa ni pamoja na vitoweo ,mchele , maharage, mafuta ya kupikia ,vinywaji na viungo vingine mbalimbali vya kupikia.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akimwakilisha Rais kukabidhi vyakula hivyo katika kituo cha kulelea watoto wanaoishi kwenye Mazingira magumu Makao ya Malezi Madina kilichopo Mtaa wa Vikawe kata ya Pangani Wilata ya Kibaha wa mkoa wa Pwani alisema kituo hicho kinawakilisha vituo 37 vilivyopo mkoa mzima.
Kunenge alisema kuwa Rais kwa kutambua makundi maalum ametoa zawadi hizo ili watoto hao washeherekee kama watakavyosheherekea wengine ambao wanaishi kwa furaha .
Nimekuja hapa leo kumwakilisha Mh.Rais wetu, amewaletea zawadi pamoja na salamu za sikukuu za mwisho wa mwaka, ambapo amewaletea
Mbuzi wawili,mchele kilo 60,maharage kilo 40, mafuta Lita 20 ,juice na viungo vingine mbalimbali"alisema Kunenge.
Aidha Kunenge alieleza ,mkoa una Jumla ya makao ya malezi 37 vyenye Jumla ya watoto 1,301, na kituo hicho kina watoto 30.
Mkuu huyo wa mkoa aliwaasa wadau wa Maendeleo na wenye uwezo kujenga tabia ya kujitolea kwa vituo vya watoto wenye mahitaji.
Kwa upande wao watoto wa Makao ya Madina Zainab Athuman na Jumanne Manzi walimshukuru Mungu kwa kumwezesha Rais kupata na kuweza kuwapa zawadi hizo.
Naye Mlezi wa watoto Makao Malezi ya Madina Fatma Abdilai alieleza wananchi waendelee kumuombea Rais Samia kwa mengi anayofanya nchini na kutekeleza ilani kwa kutambua makundi maalum.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kibaha Mjini, Mwajuma Nyamka alimshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk Samia kwa kuitendea haki ilani ya Chama na kujali watoto .






0 Comments