Header Ads Widget

MTOTO MWENYE UMRI WA MWEZI MMOJA AIBWA KAGERA.

 

NA TITUS MWOMBEKI, Matukio Daima App Kagera.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linaendelea na uchunguzi wa tukio la Wizi wa mtoto mchanga aitwae BENITA D/O BENETI,mwenye umri wa mwezi mmoja lilitokea huko katika mtaa wa Migera, Kata ya Nshambya, Tarafa ya Rwamishenyi, Manispaa ya Bukoba.


Hayo yamesemwa na Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera, William Mwampaghale-ACP wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo tarehe 01.12.2022 majira ya saa 3:30 usiku ndipo mama wa mtoto aitwae Johanitha Augustino  alipogundua kuibiwa kwa mtoto wake huyo aliyekuwa amemuacha kitandani akiwa amelala ndani ya nyumba yao.


"Ni kwamba mnamo tarehe 01/12/2022 majira ya saa 1:00 usiku watu watatu ambao ni marafiki wa mama huyo walifika nyumbani kwake kwa lengo la kumsalimia kwani walishawahi kuishi nae mtaa mmoja wa Omukigusha, Manispaa ya Bukoba"


"Mara baada ya kusalimiana na mama huyo waliaga na kuondoka na majira ya saa 3:30 usiku watu hao walirejea tena nyumbani kwa mama huyo wakiwa wawili ambapo walimwambia mama huyo wana mazungumzo nae.Mama huyo alikataa na kuahidi kufanya nao mazungumzo hayo tarehe 02/11/2022 majira ya mchana, ndipo watu hao wakamuomba mama huyo awasindikize.Mara baada ya kuwasindikiza alirejea chumbani kwake ambapo hakumkuta mtoto wake aliyekuwa amelala kitandani ndipo alibaini kuwa mtoto wake ameibiwa"


Ameongeza kuwa, Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kuwakamata watuhumiwa wote watatu ili sheria ifuate mkondo wake huku akitoa wito kwa wananchi mkoani humo watakapoona mtoto ambae wanahisi yupo na mtu au watu ambao sio wake kutoa taarifa haraka kwa Jeshi la Polisi ili hatua zichukuliwe.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI