Header Ads Widget

MILIONI 300 ZATUMIKA KUKARABATI SHULE YA SERIKALI

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Shirika la Comfort Aid International la nchini Marekani kwa kushirikiana na Taasisi ya Beta Charitable Trust ya nchini Uingereza wamekabidhi kwa uongozi wa serikali wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma  madarasa 10 ya shule ya Msingi Igalula yaliyofanyiwa ukarabati mkubwa na taasisi hizo kwa thamani ya shilingi milioni 300.

Ukarabati huo umesimamiwa na taasisi ya Bilal Muslim Tanzania chini ya Mwenyekiti wake, Mohsin Abdallah Sheni unaifanya shule hiyo kuwa shule ya mfano kwa kuwa na madarasa yenye ubora wa juu kuliko shule zote mkoani humo ikiwa pia imesaidiwa madawati mapya 500.

Katika ukarabati huo madarasa hayo yamewekewa mabati mapya ya kisasa maarufu kama Msouth, malumalu kwenye nusu ya kuta za majengo hayo ndani, nje  na kwenye sakafu, kuwekewa silingi bodi ya kisasa (Gipsam), feni za pangaboi juu na kupakwa rangi ambazo haziathiri na mvua wala jua (Weather Guard).


Ukarabati huo umekuja kufuatia kuezuliwa na mvua kwa madarasa mawili ya shule hiyo ambapo wafadhili hao kupitia Bilali Muslim Tanzania walipoombwa kusaidia uharibifu waliamua kufanya ukarabati kwa shule nzima sambamba na kujenga vyoo vya kisasa na kuiunganisha shule hiyo na mtandao wa maji safi na salama.

Mwalim Mkuu wa shule hiyo, Oscar Damian alisema kuwa mwezi Machi 17 mwaka huu madarasa mawili ya shule hiyo yaliezuliwa na mvua hali ambayo ilifanya madarasa hayo kushindwa kutumika na kuanza kuomba msaada wa namna ya kuyafanyia ukarabati.

Mwalim huyo alisema kuwa muda mfupi baada ya madarasa hayo kuezuliwa Taasisi ya Bilali Muslim Tanzania ilikuwa na ratiba ya kuzindua mradi wa maji kwenye shule hiyo ambapo wakati wa uzinduzi huo ndipo Mwalim Mkuu huyo alitoa kilio chake kwa taasisi hiyo ambayo ilitafuta wafadhili ambao wamewezesha ukarabati huo.

Kufuatia hali hiyo Mkuu wa wilaya Uvinza, Hanaf Msabaha ameishukuru Taasisi ya Bilal Muslim Tanzania kwa kuwezesha kupatikana kwa wafadhili hao ambao wamefanya ukarabati unaoacha historia kubwa kwa majengo ya mfano ya shule ya msingi ya serikali kwa mkoa huo yakiwa na ubora mkubwa kuliko shule zote za msingi na sekondari za mkoa huo.

Msabaha alisema kuwa wamejifunga jambo kubwa katika ukarabati huo na kwamba watatafuta namna ya kufanya kwenye majengo mengi ya shule zao za msingi na sekondari kuona viwango vya ubora na unadhifu wa majengo unafikia kama huo.

Mwenyekiti wa Bilal Muslim Tanzania, Mohsin Abdallah Sheni akizungumza katika makabidhiano hayo alisema kuwa ujenzi huo umwezesha na taasisi za Comfort Aid international ya Marekani na Better Charitable Ttus ya Uingereza ambao ni marafiki zake wakisaidia miradi mbalimbali ya kijamii.

Sheni alisema kuwa ukarabati huo utaiwezesha shule hiyo kudumu kwa miaka 10 bila kufanyiwa ukarabati wa rangi wala kuta zake kwani rangi iliyopigwa na malumalu zilizowekwa chini na kwenye kuta zinaweza kuoshwa kwa sabuni na uchafu kutoka.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI