Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Jeshi la polisi nchini limesema kuwa limejipanga kuimarisha ulinzi na usalama nchi nzima ili kuwawezesha watu kusherehekea sikukuu ya Chrismass na mwaka mpya kwa amani na uhuru.
Kamishna wa mafunzo na operesheni wa polini nchini,Awadhi Juma alisema kuwa ulinzi umeimarishwa nchini na kwamba wamejiweka tayari kuzima jaribio lolote linaloweza kupangwa.
Akizungumza mjini Kigoma Kamishina huyo wa polisi ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kwa kufunga nyumba zao wanapotoka kuzuia uhalifu mdogo mdogo unaoweza kujitokeza.
![]() |
"Tumejipanga vizuri kuhakikisha sikukuu hizi za mwisho wa mwaka zinafanyika kwa amani na usalama, tumepanga vijana wetu maeneo mbalimbali wakiwemo wa doria za gari na miguu hivyo sikukuu hii amani na usalama ni wa hali ya juu,"Alisema Kamishna Awadhi.
Maandalizi ya Mkesha wa Christmas yanaendelea vizuri ambapo Askofu wa Kanisa la TAG Msufini Mjini Kigoma, Omari Mlenda alisema kuwa ibada ya mkesha wa Christmass utafanyika kanisa hapo.







0 Comments