Header Ads Widget

JAMII MKOANI PWANI YATAKIWA KUSAIDIA WATU WENYE ULEMAVU.

 


JAMII Mkoani Pwani imetakiwa kuwasaidia watu wenye uhitaji wakiwemo watu wenye ulemavu ili kuwapunguzia changamoto katika maisha yao ya kila siku.

Hayo yalisemwa Mgeni rasmi kwenye sherehe za  Rahel  Chuwa ofisa maendeleo ya Jamii mkoa wa Pwani za miaka minne za Kikundi cha Wanawake cha Pwani Generation Queens zijilikanazo kama Mwanamke Sahihi Fete ambazo zilikuwa na lengo la kumkomboa mtoto mwenye ulemavu.


Chuwa alisema kuwa jamii ya watu wenye ulemavu inahitaji kusaidiwa ili nayo iweze kukufanyia shughuli zao kwa kujitegemea. 


"Watoto ni kundi ambalo linahitaji uangalizi wa karibu ambapo kwa watoto wenye ulemavu wanachangamoto nyingi zaidi hivyo wanahitaji uangalizi na usimamizi wa karibu,"alisema Chuwa.


Naye Mwenyekiti wa kikundi hicho cha Pwani Generation Queens (PGQ) cha Mkuza Wilayani Kibaha Beth Msimbe alisema wametoa viti mwendo 15 kwa watoto wenye ulemavu vyenye thamani ya shilingi milioni sita.


Msimbe alisema kuwa sherehe za kikundi hicho hufanyika kila mwaka ambapo hufanyika shughuli mbalimbali za kuisaidia jamii hasa wale wasiojiweza na wenye changamoto mbalimbali.


Alisema katika kuwezeshana wenyewe hadi sasa wamekopeshana kiasi cha shilingi milioni 74 kwa ajili ya biashara mbalimbali ambapo pia hutoa elimu ya utunzaji mazingira.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI