Wananchi mkoani Mtwara wametakiwa kuipongeza serikali Kwa Maendeleo makubwa yaliyopo katika mkoa huo hasa katika miundombinu ya barabara ambayo imepelekea mkoa huo kufikika Kwa urahisi.
Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya alisema yapo mengi yakujivunia ikiwemo ujenzi wa barabara ya uchumi ambayo awali ilitengenezwa Kwa kilomita 50 Kwa awamu ya kwanza ambapo awamu ya pili inaenda kumalizika.
Kipande kilichobakia ni kilomita 160 ambacho kikikamilika kitakuwa kimekamilisha Wilaya zote za mkoa wa Mtwara kufika kwa rami ambayo tunaamini kuwa itaongeza hamasa ya ukuaji wa uchumi"
“Serikali imeshatoa Zaidi ya shilingi bilioni 3 kwaajili ya kulipa fidia ambapo barabara hiyo itapita kwenye hizo kilomita 160 kutoka mnivata Mtwara, Tandahimba, Newala hadi Masasi"
"Sio tu kujenga barabara ya uchumi pia kuna maboresho na utanuzi wa barabara kutoka Bandari ya Mtwara hadi Mnazi mmoja ambazo ni kilomita 200 hii inatufanya tujivunie serikali yetu kwakutujali na kuendelea kutuboreshea miundombinu mbalimbali" alisema Kyobya
"Zamani ulikuwa ukitaka kutoka Mtwara kwenda mikoa mingine ilikuwa ni changamoto watu walikuwa wanalala barabarani lakini Leo miaka 61 ya uhuru tunayo barabara kiwango cha rami na pia tuna uwanja wa ndege mkubwa wenye hadhi" alisema Kyobya







0 Comments