Mheshimiwa Aziza Mangosongo, Mkuu wa Wilaya Mbinga ameongoza wananchi katika shughuli mbalimbali ili kuchochea upatikanaji wa huduma katika maeneo mbalimbali, Hivyo basi ameshiriki katika katika mambo yafuatayo;
1. *Aliongoza maandamano ya wananchi kufanya usafi katika Taasisi, masoko, stendi za magari, hospitali, ofisi, barabarani pamoja na maeneo ya makazi.* Pia, pamoja na usafi wa mazingira aliongoza zoezi la upandaji miti katika maeneo mbalimbali ili kuendelea kutunza mazingira, kulinda uoto na ikolojia. Maandamano hayo ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania bara ambayo yameanza tarehe 01/12/2022 na kilele ni tarehe 09/12/2022. Hivyo Wilaya ya Mbinga Katika wiki muhimu imejikita katika kufanya mambo mbalimbali ya kijamii.
Vilevile Mkuu wa Wilaya katika maandamano hayo aliwataka wananchi kuwa wazalendo na kuiishi Kaulimbiu ya maadhimisho haya MIAKA 61 YA UHURU: "AMANI NA UPENDO NI NGUZO YA MAENDELEO YETU" Hivyo katika kutambua umuhimu wa Uhuru ni vyema kutambua umuhimu wa kuipenda nchi kwa kuwajibika katika kufanya shughuli mbalimbali za kijamii.
2.Aliongoza kikao cha wadau wa Kilimo
ambapo Mkuu wa Wilaya alipokea taarifa kutoka kwa Maafisa wa kilimo wa halmashauri kufahamu namna huduma ya usambazaji wa pembejeo za Kilimo ulivyo kwasasa katika maeneo yao na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika utekelezaji wa zoezi hili, Vilevile alipokea taarifa kutoka kwa Chama Kikuu Cha Ushirika (MBIFACU) namna kinavyowajibika kusambaza pembejeo kwa kushirikiana na Vyama Msingi vya Ushirika (AMCOS) pamoja na changamoto zinazowakabili, Pia alipokea taarifa kutoka kwa mawakala waliopewa kibali na Serikali kutoa huduma za pembejeo kwa wakulima, Hali ya utoaji wa pembejeo na changamoto mbalimbali zinazowakabili kwasasa.
Baada ya kusikiliza, na kupokea taarifa, changamoto na maoni kutoka kwa wadau kilimo, Mkuu wa Wilaya Mbinga alieleza maazimio yafuatayo.
Aliwataka Makawala wakubwa waliopewa kibali na serikali kusambaza pembejeo wasigomee kutoa huduma kwasababu kwa kufanya hivyo wanawaumiza wakulima.
Alimtaka Meneja wa Mbifacu kushirikiana na viongozi wa vyama Msingi vya Ushirika (AMCOS) kusaidia kusambaza pembejeo katika maeneo ya karibu kwa kusajili wakulima wanaoitaji pembejeo ili kupunguza umbali na gharama za kufuata pembejeo hizo.
Aliunda kamati ndogo, Lengo la kamati hii iwasiliane na Wizara ya Kilimo moja kwa moja ili kueleza changamoto mbalimbali zilizopo ili utatuzi wa haraka ufanyike ili kukabiliana na changamoto hizo, Pia kamati iwasiliane na TRFA kuona namna ya kuongeza idadi ya Mawakala Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga hasa bonde la Hagati ambako hakuna wakala hata mmoja anayeshughulikia utoaji wa pembejeo za Kilimo. Maazimio yote yaliafikiwa na kukubaliwa na wadau wote wa Kilimo waliohudhuria katika kikao hicho Lengo ni kuhakikisha huduma hizi zinatolewa kwa ufanisi na kasi kutokana na mahitaji ya pembejeo kuwa makubwa sana huku msimu wa mvua ukiwa umeshaanza.
3. *Alishiriki Uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya siku 16 kupinga na kupambana na ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto*, Pamoja na kutoa tamko rasmi kuhusu kampeni hii ya kupinga na kupambana na ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto, Tamko hili ni "Ukatili wa Kijinsia na Ukatili dhidi ya watoto ni tatizo katika jamii na Wilaya yetu ya Mbinga. Hivyo nipende kutoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu kupinga vitendo vya ukatili kwa kuvunja ukimya na mzunguko mzima wa Ukatili, Toa taarifa mapema kwa vyombo husika, Ikiwemo dawati la jinsia la polisi, Ustawi wa jamii na idara ya Maendeleo ya jamii ili upatiwe huduma stahiki. Usiwe Muhanga, Vunja Ukimya, Ukatili wa Kijinsia unazuilika katika Wilaya yetu ya Mbinga"
Mwisho, Aliwataka Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano katika kufichua vitendo hivi vya Ukatili wa Kijinsia na Ukatili dhidi ya watoto ili kuifikia jamii yenye usawa.
0 Comments