Header Ads Widget

CHUO CHA MAFUNZO YA UHIFADHI LIKUYUSEKAMAGANGA KIMEWATAKA WAKAZI WA WILAYA NAMTUMBO KUIPONGEZA SERIKALI KWA KUIMARISHA UHIFADHI.

Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Ningu
Mkufunzi Kababi Manyonyi
Afisa masoko Irene Mville

                                                xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

                 Na Amon Mtega, Namtumbo.

MKUFUNZI na Afisa Wanyamapori Kababi Manyonyi wa Chuo cha mafunzo ya uhifadhi maliasili kwa jamii (CBCTC)Likuyusekamaganga kilichopo Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma amewataka wakazi wa Wilaya hiyo kuipongeza Serikali kwa kuimarisha uhifadhi wa maliasili kwa faida ya Jamii ikiwemo na akiba kwa  vizazi vijavyo.


Manyonyi ametoa wito huo wakati wa maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania bara ambapo katika maadhimisho hayo baadhi ya watumishi wa chuo hicho wameshiriki kongamano la pamoja na baadhi ya wakazi wa Wilaya hiyo ambalo limefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Namtumbo.


 Mkufunzi huyo akizungumza kwenye kongamano hilo ambao mgeni rasmi amekuwa mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Ningu amesema Serikali imefanikisha kuimarisha uhifadhi wa maliasili ni kutokana na ushirikishwaji kwa jamii inayozunguka maeneo ya uhifadhi kwa kupatiwa elimu juu faida za uhifadhi wa rasilimali hizo.


Manyonyi amesema kuwa kutokana na jitihada za Serikali juu ya kuimarisha uhifadhi huo ,hivyo ni vema wananchi wa Wilaya hiyo wakaendelea kuipongeza Serikali huku nao wakiendelea kuwa kipaumbele kulinda rasilimali hizo.


Aidha amefafanua kuwa hadi sasa tangu kuanzishwa kwa chuo hicho Hadi Sasa kimeshatoa wanachuo zaidi ya 5,000 ambao wamepatiwa mafunzo ya uimarishaji wa uhifadhi hapa Nchini.


Kwa upande wake Afisa masoko wa Irene Mville akizungumza kwa niaba ya mkuu wa chuo hicho Jane Nyau amesema kuwa utalii umeongezeka na Wanyamapori pia wameongezeka hivyo amesema ni jambo la kujivunia kwa faida ya vizazi vijavyo.


Mville amekitaja  chuo hicho kuwa kipo ndani ya uhifadhi ya Taifa ya Nyerere eneo la Likuyusekamaganga ili kumfanya mwanachuo aweze kujifunza kwa vitendo kwa kuzingatia uzalendo kwa jamii na kwa Taifa .


Naye mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Ningu ambaye amekuwa mgeni rasmi wakati akitoa salamu Uhuru wa Tanzania bara amesema kuwa kuna kila sababu ya kuipongeza Serikali kutokana na utendaji kazi wake wa kuwaletea maendeleo wananchi wake.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS