Header Ads Widget

CHUMBA ALICHOLALA MESSI QATAR KUWA MAKUMBUSHO

 


HATIMAYE chuo  Kikuu cha Doha (Doha University) nchini Qatar kimeweka dhamira yake ya kugeuza kuwa Makumbusho ndogo, Chumba alichokuwa anatumia kwa matumizi mbalimbali, Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi katika Michuano ya Kombe Dunia 2022 ambayo ilihitimishwa kwa Argentina kutwaa ubingwa huo.

Kupitia mitandao yao ya kijamii, Chuo Kikuu cha Qatar kimesema: “Chuo Kikuu cha Qatar kinatangaza kuwa Chumba alichokuwa anatumia Nahodha wa Argentina, Lionel Messi wakati wa Michuano ya Kombe la Dunia 2022 kitageuzwa kuwa Makumbusho ndogo.”

“Chumba cha Messi kitabaki vile vile hakibadilishwi kitu, na kitakuwa mahsusi kwa ajili ya Wageni (Watalii) na sio makazi tena, kwa kuwa tutakifanya Makumbusho ndogo ambayo itakuwa na kila kitu alichotumia Messi, tunaamini Chumba hicho kitabaki kuwa alama kwa Wanafunzi na kizazi kijacho kwa kile alichokifanya Messi kwenye Michuano ya Kombe la Dunia 2022,” amesema Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Chuo hicho, Hitmi al Hitmi.


Messi alifunga mabao saba na ‘assist’ tatu katika Michuano hiyo na kuweka rekodi ya kuwa Nyota aliyeshinda tuzo mbili za Mchezaji Bora wa Michuano hiyo (Adidas Golden Ball). Aidha, Messi amekuwa Mfungaji Bora wa muda wote katika timu ya taifa ya Argentina akimpita Mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo, Gabriel Batistuta aliyestaafu soka akiwa na mabao 10 pekee.

Nyota huyo wa PSG, imeelezwa kuwa atakuwa na mapumziko marefu ya Sikukuu baada ya kufanya kazi kubwa kwenye Michuano hiyo ya dunia, Messi atakosekana kwenye michezo miwili ya Ligi Kuu Soka nchini Ufaransa (Ligue 1) dhidi ya Strasbourg (December 28) na Lens (January 1) na huenda akawepo kwenye mchezo wa Michuano ya ‘French Cup’ dhidi ya Chateauroux, January 6.l mwaka 2023.

Hata hivyo, makazi hayo ya Chuo Kikuu cha Qatar yaliyokuwa yanatumiwa na Argentina, pia yaliwahi kutumiwa wa Klabu ya Liverpool ya Uingereza wakati inashiriki Michuano ya Kombe la Dunia ngazi ya Klabu mwaka 2019. Makazi hayo yana maeneo ya ‘Gym’ sehemu za Kuogelea (Swimming Pools) na viwanja vya mazoezi.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI