Header Ads Widget

ARGENTINA MABINGWA KOMBE LA DUNIA

 

TIMU ya Taifa ya Argentina imeibuka mabingwa kombe la Dunia kwa mikwaju ya Penati dhidi ya timu ya Taifa ya Ufaransa mara baada ya kutoka sare ya 2-2  kwa dakika 90 na 3-3 dakika 30 za nyongeza (extra time).

Argentina ilianza kutangulia kwa mabao 2-0, mabao yaliyofungwa kipindi cha kwanza kupita kwa nyota wao Lionel Messi pamoja na Angle Di Maria na kuwapeleka mapumziko wakiwa mbele.

Kipindi cha pili Ufaransa ilifanya mabadiliko ya baadhi ya wachezaji wake, mabadiliko  ambayo yalizaa matunda kwani walipata mabao mawili ya haraka kupitia kwa kijana wao nyota Kylian Mbappe na kumfanya amzidi mpinzani wake Lionel Messi kufikia mabao saba wakati mweznake akiwa na mabao sita tu kwenye michuano hiyo

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI