Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe Keneth Haule amesema hadi sasa takribani shilingi bilioni 2 za Tasaf zimetolewa kwa walengwa wa kaya masikini pamoja na kutekelezwa kwa miradi mbalimbali tangu halmashauri hiyo ianzishwe.
Taarifa hiyo ameitoa mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama akiwa mjini Makambako kutembelea miradi inayotekelezwa kupitia fedha za Tasaf na kwamba fedha hizo zimetumika kutekeleza miradi ya ujenzi wa madarasa na miundombinu mbalimbali pamoja na kuwapa walengwa wa Tasaf
Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa Tasaf Taifa Peter Lwanda amesema halmashauri ya mji wa Makambako imetekeleza miradi yake bila shaka yoyote jambo linalopaswa kuigwa na halmashauri nyingine hapa nchini.
Mbunge wa Jimbo la Makambako Deo Sanga amesema serikali imendelea kutoa fedha nyingi kuwasaidia wananchi kwani hata mpango wa Tasaf umekuwa faraja kubwa kwa wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa baada ya kutembelea miradi ya ujenzi wa nyumba ya watumishi na zahanati katika kijiji cha Ikelu amesema Tasaf wametoa fedha zinazojenga miradi mbalimbali ikiwemo ya majengo na barabara kiasi Cha zaidi ya shilingi bilioni 3 katika mji wa Makambako na kusaidia kupunguzwa kwa kero nyingi za wananchi.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama amesema fedha zinazotolewa kupitia Tasaf zinapaswa kuendelea kuwasaidia walengwa pamoja na kusaidia upatikanaji bora wa huduma za afya kwa wananchi.
Juma Mwakijege na Jenitha Mtewele ni wananchi wa Ikelu Makambako ambao wanakiri kuwapo kwa adha kubwa ya upatikanaji wa huduma za afya na kwamba sasa watakwenda kupata ahueni pindi ujenzi huo utakapokamilika.









0 Comments