Header Ads Widget

WAZAZI WAKUMBUSHWA WAJIBU WA KUSIMAMIA ULINZI WA WATOTO WAO KUZUIA UKATILI

 

Minza Edward Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Kigoma

Juma Tungilayo Mwenyekiti wa Kijiji cha Kizenga halmashauri ya wilaya Kigoma
                                    xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

WITO umetolewa kwa wazazi kuhakikisha wanasimamia malezi, matunzo na ulinzi kwa watoto wao ili kuondoa vitendo vya ukatili vinavyowatokea ikiwemo mimba kwa wanafunzi.

Afisa elimu sekondari katika halmashauri ya wilaya Kigoma, Flora Fundi alisema hayo katika mikutano ya kampeni kuhamasisha jamii kupinga vitendo vya ukatili na kusema kuwa wazazi wana mchango mkubwa wa kupunguza kama siyo kuondoa matukio ya ukatili iwapo watatimiza wajibu wao.


Fundi alisema kuwa moja ya mambo yanayowafanya watoto wengi kuingia na kuathirika na vitendo vya ukatili ni pamoja na wazazi kutozingatia kuwapangia watoto wao ratiba za matukio ya siku wala kufuatilia ratiba za watoto wao hivyo watoto kujiamulia mambo ya kufanya.


“Kuna wakati mzazi hajamuona mtoto wake hata kwa masaa matatu lakini hashituki wala kuuliza alipo na hata mtoto anaporudi mzazi hataki kujua alikuwa wapi hivyo inajenga mazoea ya watoto kujiona wako huru kufanya chochote wanachojisikia,”Alisema Flora Fundi.


Akizungumza katika mikutano hiyo ya kampeni Afisa Maendeleo ya jamii wa halmashuri ya wilaya Kigoma, Minza Edward alisema kuwa matukio ya ukatili kwa sehemu kubwa yanatokea majumbani ambako wazazi wanaishi na watoto wao na ndugu wengine.


Edward alisema kuwa pamoja na hilo wazazi wengi hawachukui jukumu la kufuatilia matendo ya watoto wao au ndugu wanaoishi nao na kwa sababu ya kuaminiwa ndugu wengine wanatumia nafasi hiyo vibaya kufanya matendo ya ukatili ikiwemo kubaka.


Akizungumza katika mikutano hiyo ya kampeni Afisa Maendeleo ya jamii wa halmashuri ya wilaya Kigoma, Minza Edward alisema kuwa matukio ya ukatili kwa sehemu kubwa yanatokea majumbani ambako wazazi wanaishi na watoto wao na ndugu wengine.


Mwenyekiti wa kijiji cha Kizenga, Juma Tungilayo alisema kuwa kamati za kupinga ukatili katika kijiji hicho zimekuwa zikikaa na kujadili mambo mbalimbali na kuchukua hatua ikiwemo wazazi kuwasimamia watoto wao lakini bado kuna shida kubwa kwa wazazi kutimiza wajibu wao.


Tungilayo alisema kuwa wazazi kushindwa kutimiza wajibu wao imekuwa chanzo cha ukatili kwa watoto ambapo vimekuwa vikitoa mwanya kwa watu wasio wema kutumia nafasi hiyo kufanya ubakaji au kuwapa mimba wanafunzi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI