Header Ads Widget

KATIBU MKUU WA CCM DANIEL CHONGOLO AFUTA NA KUSITISHA BAADHI YA CHAGUZI ZA NGAZI YA MKOA.

NA HAMIDA RAMADHANI DODOMA

CHAMA Cha Mapinduzi CCM kimefuta  uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Simiyu kutokana na wagombea kutuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa 


Pia CCM  kimesimamisha chaguzi kwa mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Mkoa wa Mbeya , Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Mkoa wa Arusha pamoja na Mkoa wa kichama wa Magharibi Unguja Zanzibar kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo Malalamiko wanachama kukimbia na box la kupigia kura lakini pia vitendo vya rushwa.


Akiongea na waandishi wa habari Jijini Dodoma Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Daniel Chongolo Amesema chaguzi hizo zimesimamishwa na kupisha uchunguzi wakina kuendelea 


"Kama tunavyofahamu Mwaka huu ni Mwaka wa uchaguzi mkuu wa Chama cha Mapinduzi wa ndani na Mimi ndio Mkurugenzi mkuu wa uchaguzi  ambapo tumeendelea kufanya uchunguzi  tangia ulivyoanza ngazi ya Shina, Tawi, kata, Jimbo, Wilaya na Sasa ngazi ya Mkoa," .


Na kuongeza" Tumekuwa tukisema Mara kwa Mara popote tutakapoona kuna changamoto tutachukua hatua na tumekuwa tukifanya hivyo kwa ngazi zote Sasa tumeshatuma tume leo hii ni siku ya tatu na tume ikimaliza  kufanya uchunguzi wake watatuletea taarifa na sisi tutafanya maamuzi , " Amesema Chongolo.


Aidha amesema Chama kimetuma  Maafisa na viongozi kuwa wasimamizi wa uchaguzi kila Mkoa hatukutaka chaguzi zifanyike bila ya macho ya maofisa na viongozi kutokuwepo.


" Nataka niseme kuwa kwa Mikoa tuliosimamisha zoezi la uchaguzi  chaguzi zingine zinaendelea kwa nafasi mojamoja  ya Mwenyekiti na nafasi zingine ambazo hazijachukuliwa hatua chaguzi zinaendelea," amesema Chongolo


Hata hivyo ameeleza Chama Cha Mapinduzi Kimekuwa kikifanya vikao na yale yote yanayohusisha mamlaka ya kikatiba zinachukuliwa hatua kwa taratibu tulizojiwekea na ndio Maana sijasema nimefuta chaguzi bali nimesimamisha kwa uchunguzi


"Changamoto ni wale wagombea au wapambe wao kuonyesha msukumo kuwa wao ndio wanaotakiwa na viongozi wa juu kuliko wengine kunawagombea wanaaojiita mgombea wa katibu mkuu,wapo wanaojiita wagombea wa Makamu na wengine kujiita wagombea wa Mwenyekiti wapo wanaojiita wagombea kamati kuu,"akisema


 "Sisi  tumeshapitisha majina Kama Mkoa fulani wawili au watatu ndio hao hao Sasa Kama nyinyi hamuwataki sisi ndio tumeshapitisha majina mkumbuke kuwa hakuna kiongozi ambaye anamgombea , "amesema.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI