Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya shirika la Lindi womene’s paralego aid centre (LIWOPAC) Afwilile Mbembela amesema ili kufikia dhamira ya kufanikisha malengo ya program ya kitaifa ya Malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT- MMMAM) ni muhimu kuzingatia ushirikishwaji na ushirikiano mzuri baina ya wasimamizi wa program, wahamasishaji pamoja na watekelezaji wa program hiyo.
Mbembela ameyasema hayo jana katika kikao kilichowakutanisha pamoja wadau wa Program hiyo kilichofanyika katika ofisi za LIWOPAC Mjini Lindi kilicholenga kuandaa tathimini ya utekelezwaji wa Program ya Kitaifa Malezi Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) katika Ngazi ya Mkoa.
Mbembela amesema kama ilivyo umuhimu wa program hiyo kujibu changamoto za mahitaji ya Watoto wadogo wenye umri kuanzia 0-8 ambapo wapo kwenye hatari ya kutofikia hatua timilifu ya ukuwaji wao kutokana na kukosa malezi bora,umasikini, utapiamlo pamoja na matatizo mengine ya kiuchumi na kijamii.
“tunapokwenda kufanya tathimini ya mradi huu kwa kuangalia shughuli zilizofanyika kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita kuanzia mwezi Julay – September itatupa picha ni kwa namna gani kila mlengwa wa program hii ni kwa namna gani ametekeleza majukumu yake”.
Alisema ni muhimu kwa watekelezaji wa program kuwafikia walengwa ambao ni Watoto kuanzi mri (0-8) , wazazi na walezi , jamii na Nchi kwa ujumla ili kuleta hamasa ya malezi makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto kwa mustakabali wa taifa imara la miaka ijayo.
Kwa upande wake Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Lindi, Gaudensia Nyamiula alisema Programu hiyo ya kitaifa ya MMMAM ni program mahususi inayoshughulikia kwa kina mahitaji ya maendeleo ya Mtoto kwa ujumla wake pamoja na kuweza kupata matokeo chanya ya utekelezaji wa afua zote za malezi jumuishi yanayoakisi mfumo mzima wa binadamu.
Alisema malengo ya Program hiyo ni kuwekeza moja kwa moja kwenye maendeleo ya mwanadamu kwa kukuza malezi jumuishi yenye tija katika uchumi kwa kuhimiza ushiriki wa sekta mbali mbali kutoa malezi jumuishi kwa kuzingatia vipengele vitano.
“vipengele hivyo ni Afya bora kwa Mtoto na malezi, Lishe ya kutosha tangu ujauzito, malezi yenye muitikio, fursa za ujifunzaji wa awali pamoja na ulinzi na usalama kwa Watoto wetu ambapo hivi vyote vikifanyika kwa pamoja mtoto anaweza kukua katika utimilifu wake” alieleza Nyamiula.
Kwa upande wake msimamizi wa Program hiyo kutoka shirika la Lindi womene’s paralego aid centre (LIWOPAC) Nellson Choaji alisema kuwa katika utekelezaji wa program hiyo unafanywa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo huku watekelezaji wakuu wa progamu wakiwa ni moaofisa kutoka katika ngazi za Halmashauri kwenye idara za maendeleo ya jamii, usawi wa jami, Lishe, Afya, pamoja na Idara ya Elimu..
Kuhusu maandalizi ya kikao cha tathimini ya unatekelezaji wa Programu hiyo ya PJT – MMMAM kinachotarajiwa kufanyika tarehe za kati kati za mwezi huu wa September Choaji alisema yamefikia Zaidi ya asilimia 70% ambapoambapo kazi inayofanyika sasa ni ukusanyaji wa Taarifa katika Ngazi ya Halmashauri kwa ajili ya kuziweka pamoja kwa ajili ya kuziwasilisha kwa wadau.
0 Comments