Header Ads Widget

VIJANA WAMUAHIDI MBUNGE ANNE KILANGO MALECELA KWENDA NAE 2025 MITANO TENA.

 


NA WILLIUM PAUL, SAME.


VIJANA wa Tarafa ya Miamba Jimbo la Same mashariki wilayani Same mkoani Kilimanjaro wamemuhakikisha Mbunge wa Jimbo hilo Anne Kilango Malecela kumchagua kwa miaka mingine mitano kuliongoza Jimbo hilo.



Vijana hao wametoa kauli hiyo mara baada ya kuona juhudi kubwa za Mbunge huyo katika kuwaletea maendeleo pamoja na kuinua vipaji vya michezo kwa kuanzisha ligi ya mpira wa miguu ya Anne Kilango cup.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Paul Ramadhani Mkazi wa kata ya Vunta alisema kuwa, toka kuchaguliwa kwa Mbunge huyo mwaka 2020 mabadiliko makubwa yameonekana katika Jimbo la Same mashariki.



Ramadhani alisema kuwa, miongoni mwa maendeleo yaliyoletwa na Anne Kilango Malecela ni pamoja na kuiboresha barabara inayoziunganisha kata za tarafa ya Miamba.


"Sisi wananchi wa Tarafa hii ya Miamba tunajishughulisha na Kilimo cha Tangawizi ambapo ndilo zao letu kubwa la kibiashara lakini tulikuwa tunakabiliwa na changamoto kubwa ya ubovu wa barabara za kutolea mazao yetu shambani hadi sokoni lakini kwa kipindi cha miaka miwili ambayo tumechagua Mbunge wetu tumeona jitihada zake katika kutatua hili" alisema Ramadhani.



Na kuongeza "Shida yetu sisi wananchi ilikuwa ni maendeleo na tumempata mtu wa kutuletea maendeleo sasa tuangaike nini tena tunakuahidi Mbunge wetu Anne Kilango Malecela mwaka 2025 tutaenda na wewe tutakupigania urudi mama yetu".


Naye Samson Mmbaga Mkazi wa kata ya Bwambo alisema kuwa, Mbunge Anne Kilango ameonyesha upendo wake mkubwa kwa vijana ambao waliukosa kwa miaka mitano 2015/2020.



Mmbaga alisema kuwa, vijana wanapenda sana michezo kwani mbali na kujenga mwili pia inatoa ajira hivyo kitendo cha Mbunge huyo kuthamini michezo kwa kuanzisha ligi ni kuonyesha jinsi anavyojali ndoto za vijana wa Jimbo la Same mashariki.


Ligi ya mpira wa miguu ya Anne Kilango cup iliyofungwa juzi katika Tarafa ya Miamba inatarajiwa kuanza katika Tarafa ya Gonja na badae kumalizikia Tarafa ya Ndungu.

Mwisho...

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI