Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya mapato Tanzania TRA Mkoa wa Mtwara wakishirikiana na wananchi na taasisi zingine wamefanya usafi katika
maeneo mbalimbali kata ya Chikongola Manispaa ya Mtwara Mikindani ili
kuweza kuhamasisha ufanyaji wa usafi kwa wakazi wa maeneo hayo.
Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya shukrani kwa mlipakodi
Kaimu Meneja wa TRA Mkoa wa Mtwara Elirehema Kimambo alisema kuwa
wamefanya usafi ili kweza kuhamasisha jamii kuwa na utaratibu wa
kulipa kodi.
“Sisi ni sehemu ya jamii siku hii ni muhimu kwetu ili kujenga uhusiano
wa karibu kati yetu na wafayabishara na kuonyesha kwamba zoezi la
kukusanyaji wa kodi ni zoezi letu ni kwaajili ya kupendezesha mji wetu
wa Mtwara” alisema Kimambo
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya aliagiza zoezi hilo kufanyika
kila jumamosi.
“Zoezi lifanyike kila jumamos nitambue kazi nzuri inayofanywa na TRA
ambapo wanarudisha faida wanayoipata kupitia ulipaji kodi tunaoufanya
naamini maeneo yaote ya masoko yatawekwa dustben ili mtu aweze kutupa”
Nataka hili zoezi la usafi liwe endelevu kwa kila kata elimu ya usafi
itolewe kwa wananchi vizimba vitolewe uchafu ili kutoa nafasi ya
kuhifahdi uchafu mwinginen kwa wakati” alisema Kyobya
Kwa upande wake mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Kanal
Emmanuel Mwaigobeko alisema kuwa wataendela kufanya usafi kila
jumamosi ili kuweka mji huo katika hali ya usafi.
“Hili zoezi ni zuri na litakuwa endelevu tunaamini kuwa tutapanga kila
jumamosi tuwe tunafanyausafi ili kuifanya jamii yetu kuwa katika
mwonekano mzuri kwa kuhama kata hadi kata” alisema Kanal Mwaigobeko
Nae Diwani wa kata ya chikongola mussa Namtema alisema kuwa suala la
usafi limekuwa ni desturi kwa ofisi yake kuhamasisha wananchi hivyo
kupitia zoezi hilo wananachi wengi watajifunza.
“Tulikuw atunafanya usafi kila baada ya wiki mbili na zoezi endelevu
tumeona hamasa kubwa itakuwa aibu taasisi iwe na uchafu mbele yake
chukueni hatua imeonyeshwa wananchi” alisema Namtema
MWISHO








0 Comments