Header Ads Widget

ST. MATTHEW'S KUTOA ELIMU KIDIGITALI MWAKANI

 


Uongozi wa shule za St. Matthews katika mikoa ya Dar es salaam, Pwani na iringa umesema wameanza kubadili mfumo wa ufundishaji kutoka kutumia chaki na ubao hadi kutumia computa kwa lengo la shule hizo kutoa elimu kidigitali zaidi kufikia viwango vya kumataifa.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa shule hizo za St. Matthews Peter Tadeus Mutembei wakati akitoa taarifa kwenye mahafari ya 21 ya shule ya Sekondari ya Ujenzi iliyopo Mkuranga mkoani Pwani.


Alisema tayari mabadiliko hayo yameshaanza kutekelezwa katika baadhi ya madarasa hadi malengo yatakapotimia kwa kuhakikisha madarasa yote yanapata runinga ifikapo mwaka 2023.



Peter ameishukuru serikali kwa kuruhusu mfumo wa kidigitali katika utoaji wa elimu mashuleni ambao umekuwa ukirahisisha usomaji kwa wanafunzi nchini.


Alisema "Ulinwengu unabadilika Sasa hivi ambapo sayansi na teknojia vinakuwa kwa kasi sana hivyo na shule hizo zimeanza kubadili mfumo wa ufundishaji kutoka kutumia chaki na ubao hadi kutumia kompyuta na TV".


Peter amesema uongozi wa shule hizo umedhamiria kutoa huduma kwa kutoa elimu kwa Watoto wa kitanzania nchini na sio kufanyabiashara kwa lengo la kuchochea ukuwaji wa maendeleo ya elimu nchini kwa kuchochea taaluma Bora kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kutoa stadi za kazi kwa wanafunzi kuwajengea uwezo wa kuajiriwa na kujiajiri katika maisha yao.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI